ads

Wednesday, 14 March 2018

YESU NAKUPENDA BY: ROSE MUHANDO







Chorus:
Yesu wee nakupenda, bwana yesu wee nakupenda,x2
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda,
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda,
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda,
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda,
Yesuuuu, yesu.

Msalabani dhambi zangu ulichukua,
Kufika kalivari Bwana ulizitua
Nami niwekwa huru ninakwimbia, (Repeat)

Nikufananishe na nani mwokozi wangu?
Naona fahari mimi ninakuimbia,
Nani asimame badala yako?
Hakuna mwingine ni wewe pekee yako.(Repeat)

Nafahamu Yesu anipenda mimi.

Chorus:
Yesu wee nakupenda, bwana yesu wee nakupenda,x2
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda,
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda,
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda,
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda,
Yesuuuu, yesu.

Nilipokuwa kwa shetani niliugua,
Ndugu na jamaa zangu walinikimbia,
Lakini yesu wa huruma ukanihurumia,
Nikufananishe na nani mwokozi wangu?
Naona fahari mimi ninakuimbia,
Nani asimame badala yako?
Hakuna mwingine ni wewe pekee yako.

Nafahamu Yesu anipenda mimi.

Chorus:
Yesu wee nakupenda, bwana yesu wee nakupenda,x2
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda,
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda,
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda,
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda,
Yesuuuu, yesu.


Kwimake eeh, kwimake weh,Kwimake weeh, kwimake eh
Kwimake mundewa Yesu,oh kwimake eh
kunilapa kwe ruhoma baba, oh kwimake weh
kunilapa kwe ruhoma baba, oh kwimake weh
Kwimake baba, kwimake baba, Kwimake baba, kwimake baba
Kwimake mundewa baba,oh kwimake eh
Jaga kyala, jaga kyala, jaga kyala baba, jaga kyala
Asante mwokozi wangu, uh asante eh,Asante mwokozi wangu, uh asante eh




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







UTAMU WA YESU BY: ROSE MUHANDO







Lile lile,

Acheni muone utamu wa Yesu we,
Mama we onjeni utamu wa Yesu we,
Mwenzenu nimeonja utamu wa Yesu we,
Usione nina raha nimeonja utamu wa Yesu we,
Si kama nimechanganyikiwa bali ni utamu wa Yesu we,
Jamani sijarukwa na akili bali utamu wa Yesu we,
Utamu we, nimeonja utamu we x2

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2
Utamu we, utamu x3
Utamu wa Yesu we, he
Mwemere, mwemere x4 (?)

Viko vingi vitamu lakini mwisho wake mauti,
Viko vingi vitamu lakini mwisho wake kilio,
Vingine ni vitamu lakini mwisho wake kilio,
Ni vitamu lakini mwisho vichungu kama shubiri,
Ni vitamu lakini mwisho vinawasha kama upupu,
Ni vitamu lakini mwisho vinapalia we,
Acheni niuseme utamu wa Yesu we,
Wacheni nisifu utamu wa Yesu we,
Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we,
Haufanani na utamu wa asali, utamu wa Yesu we,
Thamani yake imeshinda almasi, utamu wa Yesu we,
Ni mali ghafi isiopatika kwa mapesa jamani he,
Bali kwa njia ya msalaba tumepewa utamu wa Yesu we,
Mbinguni tunakwenda bure, uzima tunapata bure,
Wokovu tumepata bure, amani tunapata bure,
Utamu we, nimeonja utamu we x2

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2
Utamu we, utamu x3
Utamu wa Yesu we, he
Mwemere, mwemere x4 (?)

Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we,
Usione tuna raha, tumeonja utamu wa Yesu we,
Usione tunacheka, tumeonja utamu wa Yesu we,
Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we,
Umetusogeza karibu na Mungu, utamu wa Yesu we,
Dhambi zetu zimewekwa mbali na Mungu, utamu wa Yesu we,
Walio chini wameinuliwa, utamu wa Yesu we,
Badala ya kilio ni kicheko, utamu wa Yesu we,
Badala ya aibu utukufu, utamu wa Yesu we,
Mito ya baraka inatiririka, utamu wa Yesu we x2
Utamu we, nimeonja utamu we

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2
Utamu we, utamu x3
Utamu wa Yesu we, he
Mwemere, mwemere x4 (?)

Mkitaka magari mazuri, onjeni utamu wa Yesu we,
Mkitaka majumba mazuri, onjeni utamu wa Yesu we,
Mkitaka kubarikiwa, onjeni utamu wa Yesu we,
Mkitaka kuinuliwa, onjeni utamu wa Yesu we,
Utamu we, nimeonja utamu we.

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







UNASHANGAZA BY: ROSE MUHANDO







Tu-ru tururu tu-ru (?)

Matendo yako ya ajabu, yashangaza,
Fadhili zako za milele Baba, zashangaza,
Nikitazama ulivyoumba, ya shangaza,
Upendo wako kwangu mimi, yashangaza,
Miijuza na maajabu tele, washangaza,
Wanyama wa kondeni Baba, washangaza,
Milima na mabonde inaimba, washangaza,
Wanyama nao wanasema wewe washangaza,
Uumbaji wako Mungu, washangaza.

Matendo yako ya ajabu, washangaza,
Fadhili zako za milele Baba, zashangaza,
Uwezo wako kwa ulimwengu, washangaza,
Uumbaji wako wa pekee, washangaza,
Nikupe nini Mungu wangu? Washangaza,
Unavyonipigania Baba, washangaza,
Neema zako kwangu mimi, yashangaza.

Refrain: Ni wewe, ni wewe,
Mataifa waimba, niwewe,
Mbingu zaimba,
..?.. imba,
Jerusalemu waseme,
Mwenye nguvu ni wewe,
Mwenye uwezo ni wewe,
Wateule na waimbe,
..?.. imba,
..?.. imba,
Wateule imbeni,
Mwenye nguvu ni wewe,
Mwenye uwezo ni wewe,
Mwenye mamlaka,
Mungu nani kama wewe?






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







NIPISHE NIPITE BY: ROSE MUHANDO







Verse 1:
Nakuuliza shetani umepata wapi mamlaka,
Ya kukamata akili za watu,
Wewe umeleta balaa umeingia makanisani,
Umekamata wababa wanabaka watoto wao,
Umekamata vijana umewatwika ulevi,
Bila kusahau kina mama, vikao vya masengenyo,
Sasa nimechoka na mambo yako,
Ewe shetani, nipishe nipite.

Chorus:
Wewe ulimwasi mungu, nipishe nipite,
Uliwadanganya adamu na Eva, songea nipite,
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako,
WEwe ulimwasi mungu, nipishe nipite,
Uliwadanganya Adamu na Eva, songea nipite,
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako,
wewe shetani unaambiwa, mwenyeji wa kuzimu,
Sasa nipishe nipite.

Verse 2:
Hebu nipishe nipite, ninachelewa njiani,
Yesu yu karibu kurudi, kulichukua kanisa,
Kanda unayo nionyesha yote yamepitwa na wakati,
Huna ujanja,
Kumbuka miaka elfu mbili iliyopita zamani,
Yesu aliposhuka kuzimu, akakunyanganya funguo,
Funguo za mamlaka,
Nasema nimechoshwa na mambo yako,
Wewe shetani nipishe nipite.

Chorus:
Wewe ulimwasi mungu, nipishe nipite,
Uliwadanganya adamu na Eva, songea nipite,
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako,
WEwe ulimwasi mungu, nipishe nipite,
Uliwadanganya Adamu na Eva, songea nipite,
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako,
wewe shetani unaambiwa, mwenyeji wa kuzimu,
Sasa nipishe nipite.

Verse 3:
Nakuamuru shetani wewe, nipishe nipite,
Wewe umekuwa ni kikwazo kwangu, Kufika mbinguni,
Muda wako umeshakwisha, songea nipite,
Sasa haleluya naenda mbinguni, hakuna mashaka.
(Repeat)

Verse 4:
Wewe ulishaaniwa, laana milele,
Ulinyanganywa mamlaka na Yesu, Huna ujanja ee,
Simba wa yuda aliponguruma, mafuriko kuzimu,
Sasa haleluya twaenda mbinguni, hatuna mashaka.
(Repeat)

Chorus:
Wewe ulimwasi mungu, nipishe nipite,
Uliwadanganya adamu na Eva, songea nipite,
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako,
WEwe ulimwasi mungu, nipishe nipite,
Uliwadanganya Adamu na Eva, songea nipite,
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako,
wewe shetani unaambiwa, mwenyeji wa kuzimu,
Sasa nipishe nipite.






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







NALEGEA BY: ROSE MUHANDO







{Nalegea, wacha nichakae nje,
Lakini utu wangu wa ndani wa fanywa upya}x2
{Dhiki yangu ni nyepesi na ya muda,
Yaani fani wa utukufu wa milele} x2
{Nayahesabu mambo yote bure,
Kwa ajili ya jina la Yesu (Kristo)} x2

{Natazama, tena imeandikwa,
Ni mizuri kama nini – miguu yao} x2
{Wale wote wapelekeo habari njema,
Ya utukufu wa Yesu Kristo Bwana wangu} x2
{Nayahesabu mambo yote kama mavi/bure,
Kwa ajili ya uzuri wa Yesu (Kristo)} x2

Vipi mwenzangu, wanitazama?
Ninaposema habari zako,
Ninapotaja na mambo zako,
Wacha Makali, hasira nyingi,
{Wazielekeza juu yangu, bila sababu,
Na kumbe mimi ni mtumishi, niliyetumwa} x2

Nikikwambia uache dhambi,
Ushirikina, uchawi fitina,
Wanichukia, wanichukia,
{Lakini Bwana asema hivi, ni ole wenu,
Wanawake washonao hirizi viunoni mwao,
Wanaoroga kwa mafumbo, wasio na haya} x2

{Sikia, ewe mkaidi,
Ee mwenye shingo ya chuma,
Utavuna ulichopanda,
Mabaya yatakupata} x2

{Kumbuka ewe mshirikina:
Uzao wa mwanamke mchawi,
Mumeo atatwaliwa,
Wanao watabaki yatima,
Na uchawi, hautakusaidia} x2

{Ninawaangalia yatima,
Ninawafahamu wajane,
Nimesikia kilio chao,
Nimeyaona mateso yao} x2

{Lakini Yesu, amefukuka,
Dhambi, mauti hakuna tena,
Shetani kuzimu, anatetemeka} x2

{Eh Halleluya, sasa twashinda,
Mapendo yakimbia kwa jina lake} x2

Wewe, Yesu ni njia,
Wewe, Yesu ni uzima.




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







MUNGU WANGU BY: ROSE MUHANDO







E mungu wangu mimi ninatukushukuru,
Mbele ya mataifa mimi nitaimba,
Dunia nzima nayo itambue hilo,
Kwamba jina la yesu pekee ndilo,
Ulimwengu mzima uokolewe kwalo.

Asubuhi na mapema, mimi nitaimba,
Kabla ya kinywa kunena, kwako nitaimba,
Tufani ijapozidi wo, kwako nitaimba,
Nijapoteswa kabisa, kwako nitaimba,
Nijapodharauliwa, kwako nitaimba.

Chorus:
Swiyi… Sikia e kinanda,
Swiyi… Amka we kinubi,
Swiyi… Sikia e kinanda,
Inuka e zumari, inuka kwa sauti(x2)
Woo na utukuzwe Mungu, Woo na utukuzwe Mungu,
Yee Jehova adonai, Yee Jehova adonai,
El gibo shalom mungu unaitika
El gibo shalom mungu unaitika

Uniondolee majivuno, komesha kiburi,
Utawale akili zangu, Bwana niongoze,
Unifundishe roho yangu habari za mbingu,
Sikizeni eh kizazi changu, Mungu anaishi,
Uniondolee majivuno, komesha kiburi,
Utawale akili zangu, Bwana niongoze,
Unifundishe roho yangu habari za mbingu,
Sikizeni eh kizazi changu, Mungu anaishi.

Chorus:
Swiyi… Sikia e kinanda,
Swiyi… Amka we kinubi,
Swiyi… Sikia e kinanda,
Inuka e zumari, inuka kwa sauti(x2)
Woo na utukuzwe Mungu, Woo na utukuzwe Mungu,
Yee Jehova adonai, Yee Jehova adonai,
El gibo shalom mungu unaitika
El gibo shalom mungu unaitika.

NIpe moyo ya nyama, ulopondeka,
Moyo uliotulia, na unyeyekevu,
Mimi si kitu kwako, ni mdhuru? tu,
Mimi ni kama nani, uniinue,
Unifinyange bwana, kama upendavyo,
Unifundishe Bwana kama upendavyo.

Chorus:
Swiyi… Sikia e kinanda,
Swiyi… Amka we kinubi,
Swiyi… Sikia e kinanda,
Inuka e zumari, inuka kwa sauti(x2)
Woo na utukuzwe Mungu, Woo na utukuzwe Mungu,
Yee Jehova adonai, Yee Jehova adonai,
El gibo shalom mungu unaitika
El gibo shalom mungu unaitika

NIkikuita mungu, unaitika,
Rohi eloie heika (?), noishikimu (…Hebrew (?))
Jira el shadai, Jehova oseenu(…Hebrew (?))
El elyo shammah, Mungu unaitika,
Jehova shabbah, Mungu utanijibu,
El gibo shalom, Mungu unaitika,
El gibo shalom, Mungu unaitika,
El gibo shalom, Mungu unaitika.

Chorus:
Swiyi… Sikia e kinanda,
Swiyi… Amka we kinubi,
Swiyi… Sikia e kinanda,
Inuka e zumari, inuka kwa sauti(x2)
Woo na utukuzwe Mungu, Woo na utukuzwe Mungu,
Yee Jehova adonai, Yee Jehova adonai,
El gibo shalom mungu unaitika
El gibo shalom mungu unaitika






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







NAKAZA MWENDO BY: ROSE MUHANDO







Nafurahia mateso yangu, nafurahia mateso yangu,
Ujapoharibika mwili huu, tapata mwingine kwa Baba,
Ujapoharibika mwili huu, tapata mwingine kwa Baba.

Chorus:
Nakaza mwendo, nifike Mbinguni,
Nayakabidhi, maisha kwa Bwana,
Nauone, uzuri wa bwana.x2

Taabu na matatizo, hakuna,
Kiu wala njaa, hakuna.x2

Verse 2:
Lakini mji ule taa yake, ni mwana kondoo,
Milele mji ule hauitaji, jua wala mwezi.

Najua kuishi kwangu ni pigo, kufa ni faida,

Chorus:
Nakaza mwendo, nifike Mbinguni,
Nayakabidhi, maisha kwa Bwana,
Nauone, uzuri wa bwana.x2

Verse 3:
Lakini waongo na wazinzi, hawataingia,
wala waabudu sanamu, hawataingia.x2

Najua kuishi kwangu ni pigo, kufa ni faida,

Chorus:
Nakaza mwendo, nifike Mbinguni,
Nayakabidhi, maisha kwa Bwana,
Nauone, uzuri wa bwana.x2






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







KIATU KIVUE BY: ROSE MUHANDO







Mungu alinena naye Musa hicho kiatu kivue,
Mungu alinena naye Musa hicho kiatu kivue,
Ulichotoka nacho kwa farao nakwambia,
Pahali hapa ni patakatifu hicho kiatu kivue. (x2)

Musa hicho kiatu, Musa hicho kiatu,
Nataka ninene nawe, nataka nikutumie,
Nataka nikuinue, nataka nikubariki,
Watu wangu waangamia,taifa langu la Israeli,
Watu wangu wanasononeka,watu wangu wanateseka,
Nataka nikutumie wewe, ukaokoe taifa langu we.

Hata leo mungu anena nasi hicho kiatu we,
Kiatu ni dhambi uzifanyazo ninakwambia,
Ukahaba unaoeneza kando kando ni kiatu,
Wivu na masengenyo vimekuja ni kiatu,
Kitakupeleka jehanamu hicho kiatu,
Kitakupeleka motoni wewe hicho kiatu,
Uzinzi unaoeneza wewe ni kiatu,
Uvalie wake wa wenzio magoti we nakwambia,
Utongoza waume wa wenzio ni kiatu we,
Kitakupekea jehanamu hicho kiatu,
Mama hicho kiatu, baba hicho kiatu,
Nataka ninene nawe, maana ninakupenda,
Nataka ninene nawe, ili nikuokoe,
Mimi sitaki uangamie, mimi sitaki upotee,
Mimi sitaki uangamie, maana mimi ninakujali,
Mimi Mungu ni wa neema, mimi mungu ni wa upendo.

Ukitaka Mungu akubariki lazima kiatu kivue,
Ukitaka kuinuliwa wewe ni lazima kivue,
Wivu ulio nao wewe ni lazima kivue,
Hutaki kuona mwenzako mama akiinuliwa wewe,
Hutaki kuona mwenzako akiwa amependeza,
Hutaki kuona mwenzako akiwa yuko smart,
Tabia ulio nayo mama ninakwambia wewe,
Hutaki kuona ndoa ya mwenzako jamani mke na mume wakicheka,
Tabia uliyo nayo baba, nakwambia badilika,
Hutaki kuona huduma ya mwenzako jamani likisonga mbele,
Hebu kivue, jamani hebu kivue,
Kiatu cha nyumba ndogo, kiatu cha ulevi,
Kiatu cha uzinzi, kiatu cha masengenyo,
Kivue, kivue, kivue, kivue.

Mungu ananena nawe hicho kiatu kivue,
Mungu anena nawe hicho kiatu kivue,
Valia mini waume wa wenzio iwe mwisho,
Kuvalia vitovu waume wa wenzio iwe mwisho,
Kupaka wanja kwa waume wa wenzio iwe mwisho,
Nataka nikupe mumueo, nataka nikupe nyumba yako,
Nataka nikuinue, nataka nikuinue,
Nataka nikuinue, niinue mume wako,
Niinue nyumba yako, nimwunue mke wako,
Nikupatia mchumba, kiatu cha nyumba ndogo,
Mungu anasema nawewe hicho kiatu kivue,
Kivue, kivue, kivue, kivue,
Ah, hicho kiatu kivue






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







UTUKUZWE BY: ROSE MUHANDO







Ee Mungu utukuzwe, milele na milele,
Tena uinuliwe, katika mataifa yote,
Ee Mungu utukuzwe, milele na milele,
Ee Mungu uinuliwe, milele na milele,
Tena uhimidiwe katika mataifa yote,
Jina lako la ajabu, Wewe utishaye kuliko. x2

Wala haufanananishwi na chochote,
Jina lako Baba la ajabu.

Refrain:
Wewe uliupiga mwamba (maji yakabubujika),
Katikakati ya jangwa (wewe ulifanya njia),
Walipokumbana na adui (Wewe uliwapigania)
Wakafika (Kule Kanaani salama) X2
Usifiwe, utukuzwe, x2
Utukufu ni wako, milele na milele X2

Haya visiwa na viimbe,
Mito na ipige makofi,
Ndege na waseme amina kubwa,
Wanyama wa mwitu wasifu, X2
Bwana anatawala/Maana unatawala, wewe Bwana,
Heshima na enzi ni vya Bwana,
Utukufu na nguvu ni vya Bwana,
Umeketi mkono wenye nguvu, X2

Refrain:
Wewe uliupiga mwamba (maji yakabubujika),
Katikakati ya jangwa (wewe ulifanya njia),
Walipokumbana na adui (Wewe uliwapigania)
Wakafika (Kule Kanaani salama) X2
Usifiwe, utukuzwe, x2
Utukufu ni wako, milele na milele X2

Heshima ni yako (milele na milele),
Utukufu ni wako (milele na milele),
Heshima ni yako (milele na milele),
Mamlaka ina wewe (milele na milele),
Malaika waimbe (milele na milele),
Wazee ishirini na nne waseme (milele na milele),
Na wale wenye uhai waimbe (milele na milele),
Na watakatifu waseme (milele na milele).




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







SITANYAMAZA BY: ROSE MUHANDO







Eeeehhhh…. Mimi Mungu (Me, God)
Matendo nitalia, Kwa sinani nitaomboleza
Sodoma nitanung’unika, Mipakani nitashambulia
Mijini wameniacha,Kila mara nitashambulia
Maisha ya wanadamu, Yamenichosha….

Oh oh mimi
Sitanyamaza, wala sitanyamaza
Lakini nitalipa ujira wa vifuani mwao
Maovu yenu ninyi, pamoja na baba zenu
nasema nitalipa ndio mjue mimi ni Bwana
Mmefukiza uvumba, na kunitukana
Kwa ajili ya haya mtajutia vitani mwenu?(repeat)

mmefanya uzinzi katikati ya milima
Usiku wa manane mmefanya ukahaba
Kwenye njia kuu na vichochoro mmefanya mapatano
Kwenye mialoni na mipera mmefanya machukizo (repeat)

Ulitumaini uzuri wako ukafanya ukahaba
Kila kijana aliyepita ulimwona anafaa
Awe mzuri na sura mbaya ulifunua marinda

Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda
Wako wapi mapenzi zako mbona sasa unakonda
Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda
Wako wapi waelizamu (?) wako mbona sasa unakonda

Miji mizuri imekuwa ukiwa
Majumba mazuri yamefungwa kabisa
Wana wa wana wamebaki yatima
Kiburi chamuwamu(?) imekoma kabisa (repeat)

Hebu sasa piga kelele uliye kahaba,
Shika kinubi omboleza upate kukumbukwa (repeat)

Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye
Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye (repeat)

Lakini Bwana asema hivi, nitawaponya
Yeye mwenyewe aahidi, nitawabariki
Mimi ni alfa na omega, mwanzo na mwisho
Jamani mimi ni mungu, mwingine hapana

Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye (repeat)




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site