ads

Wednesday 14 March 2018

KIATU KIVUE BY: ROSE MUHANDO







Mungu alinena naye Musa hicho kiatu kivue,
Mungu alinena naye Musa hicho kiatu kivue,
Ulichotoka nacho kwa farao nakwambia,
Pahali hapa ni patakatifu hicho kiatu kivue. (x2)

Musa hicho kiatu, Musa hicho kiatu,
Nataka ninene nawe, nataka nikutumie,
Nataka nikuinue, nataka nikubariki,
Watu wangu waangamia,taifa langu la Israeli,
Watu wangu wanasononeka,watu wangu wanateseka,
Nataka nikutumie wewe, ukaokoe taifa langu we.

Hata leo mungu anena nasi hicho kiatu we,
Kiatu ni dhambi uzifanyazo ninakwambia,
Ukahaba unaoeneza kando kando ni kiatu,
Wivu na masengenyo vimekuja ni kiatu,
Kitakupeleka jehanamu hicho kiatu,
Kitakupeleka motoni wewe hicho kiatu,
Uzinzi unaoeneza wewe ni kiatu,
Uvalie wake wa wenzio magoti we nakwambia,
Utongoza waume wa wenzio ni kiatu we,
Kitakupekea jehanamu hicho kiatu,
Mama hicho kiatu, baba hicho kiatu,
Nataka ninene nawe, maana ninakupenda,
Nataka ninene nawe, ili nikuokoe,
Mimi sitaki uangamie, mimi sitaki upotee,
Mimi sitaki uangamie, maana mimi ninakujali,
Mimi Mungu ni wa neema, mimi mungu ni wa upendo.

Ukitaka Mungu akubariki lazima kiatu kivue,
Ukitaka kuinuliwa wewe ni lazima kivue,
Wivu ulio nao wewe ni lazima kivue,
Hutaki kuona mwenzako mama akiinuliwa wewe,
Hutaki kuona mwenzako akiwa amependeza,
Hutaki kuona mwenzako akiwa yuko smart,
Tabia ulio nayo mama ninakwambia wewe,
Hutaki kuona ndoa ya mwenzako jamani mke na mume wakicheka,
Tabia uliyo nayo baba, nakwambia badilika,
Hutaki kuona huduma ya mwenzako jamani likisonga mbele,
Hebu kivue, jamani hebu kivue,
Kiatu cha nyumba ndogo, kiatu cha ulevi,
Kiatu cha uzinzi, kiatu cha masengenyo,
Kivue, kivue, kivue, kivue.

Mungu ananena nawe hicho kiatu kivue,
Mungu anena nawe hicho kiatu kivue,
Valia mini waume wa wenzio iwe mwisho,
Kuvalia vitovu waume wa wenzio iwe mwisho,
Kupaka wanja kwa waume wa wenzio iwe mwisho,
Nataka nikupe mumueo, nataka nikupe nyumba yako,
Nataka nikuinue, nataka nikuinue,
Nataka nikuinue, niinue mume wako,
Niinue nyumba yako, nimwunue mke wako,
Nikupatia mchumba, kiatu cha nyumba ndogo,
Mungu anasema nawewe hicho kiatu kivue,
Kivue, kivue, kivue, kivue,
Ah, hicho kiatu kivue






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







No comments:

Post a Comment