ads

Monday 9 January 2017

AMINI - GLORIA MULIRO











Verse 1:
Tangu niwe mdogo, ni mengi nimepita,
Mengine mazuri, mengine machungu,
Lakini jambo moja ninalijuwa,
Heri mwisho wa jambo, kuliko mwanzo wake.

Chorus:
Amini mwenzangu (Mungu atakuweka juu),
Amini moyoni (Mungu atakuweka juu),
Usiwe na shaka (Mungu atakuweka juu),
Usiwe na hofu (Mungu atakuweka juu),
Hata kama uko chini (Mungu atakuweka juu),
Hata kama umeshindwa (Mungu atakuweka juu),
Usiwe na shaka (Mungu atakuweka juu),
Usiwe haraka (Mungu atakuweka juu).

Verse 2:
Mwanzo nilivyokuwa, mimi sikuchagua,
Yote niliyopitia, mimi sikuchagua,
Kukosa chakula, mavazi, amani sikuchagua,
Kudharauliwa, kuteseka, kupotea njia sikuchagua,
Ila Nashukuru Mungu alitumia yote kunitengeneza.

Chorus:
Amini mwenzangu (Mungu atakuweka juu),
Amini moyoni (Mungu atakuweka juu),
Usiwe na shaka (Mungu atakuweka juu),
Usiwe na hofu (Mungu atakuweka juu),
Hata kama uko chini (Mungu atakuweka juu),
Hata kama umeshindwa (Mungu atakuweka juu),
Usiwe na shaka (Mungu atakuweka juu),
Usiwe haraka (Mungu atakuweka juu).

Verse 3:
Mwanzo wako najua haukuchagua,
Japo mambo uliyopita wewe hukuchagua,
Lakini amini hayo Mungu anakwambia,
Macho hayajaona masikio hayajasikia,
Mambo makubwa amekupangia.

Chorus:
Amini mwenzangu (Mungu atakuweka juu),
Amini moyoni (Mungu atakuweka juu),
Usiwe na shaka (Mungu atakuweka juu),
Usiwe na hofu (Mungu atakuweka juu),
Hata kama uko chini (Mungu atakuweka juu),
Hata kama umeshindwa (Mungu atakuweka juu),
Usiwe na shaka (Mungu atakuweka juu),
Usiwe haraka (Mungu atakuweka juu).




www.gospelyrix.com







No comments:

Post a Comment