ads

Monday 9 January 2017

UTAMU WA YESU BY ROSE MUHANDO











Lile lile,

Acheni muone utamu wa Yesu we,
Mama we onjeni utamu wa Yesu we,
Mwenzenu nimeonja utamu wa Yesu we,
Usione nina raha nimeonja utamu wa Yesu we,
Si kama nimechanganyikiwa bali ni utamu wa Yesu we,
Jamani sijarukwa na akili bali utamu wa Yesu we,
Utamu we, nimeonja utamu we x2

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2
Utamu we, utamu x3
Utamu wa Yesu we, he
Mwemere, mwemere x4 (?)

Viko vingi vitamu lakini mwisho wake mauti,
Viko vingi vitamu lakini mwisho wake kilio,
Vingine ni vitamu lakini mwisho wake kilio,
Ni vitamu lakini mwisho vichungu kama shubiri,
Ni vitamu lakini mwisho vinawasha kama upupu,
Ni vitamu lakini mwisho vinapalia we,
Acheni niuseme utamu wa Yesu we,
Wacheni nisifu utamu wa Yesu we,
Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we,
Haufanani na utamu wa asali, utamu wa Yesu we,
Thamani yake imeshinda almasi, utamu wa Yesu we,
Ni mali ghafi isiopatika kwa mapesa jamani he,
Bali kwa njia ya msalaba tumepewa utamu wa Yesu we,
Mbinguni tunakwenda bure, uzima tunapata bure,
Wokovu tumepata bure, amani tunapata bure,
Utamu we, nimeonja utamu we x2

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2
Utamu we, utamu x3
Utamu wa Yesu we, he
Mwemere, mwemere x4 (?)

Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we,
Usione tuna raha, tumeonja utamu wa Yesu we,
Usione tunacheka, tumeonja utamu wa Yesu we,
Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we,
Umetusogeza karibu na Mungu, utamu wa Yesu we,
Dhambi zetu zimewekwa mbali na Mungu, utamu wa Yesu we,
Walio chini wameinuliwa, utamu wa Yesu we,
Badala ya kilio ni kicheko, utamu wa Yesu we,
Badala ya aibu utukufu, utamu wa Yesu we,
Mito ya baraka inatiririka, utamu wa Yesu we x2
Utamu we, nimeonja utamu we

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2
Utamu we, utamu x3
Utamu wa Yesu we, he
Mwemere, mwemere x4 (?)

Mkitaka magari mazuri, onjeni utamu wa Yesu we,
Mkitaka majumba mazuri, onjeni utamu wa Yesu we,
Mkitaka kubarikiwa, onjeni utamu wa Yesu we,
Mkitaka kuinuliwa, onjeni utamu wa Yesu we,
Utamu we, nimeonja utamu we.

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2




www.gospelyrix.com







No comments:

Post a Comment