HACHAGUI - ESTHER WAHOME
Chorus:
Naendelea mbele, naendelea mbele,
Sirudi nyuma tena, naenda na Yesu.[Repeat]
Verse 1:
Mengi nimeona, ya kunivuta nyuma,
Ewe Bwana Yesu, umenisaidia,
Sio kwa nguvu, wala mamlaka,
Bali ni kwa Roho, wako mtakatifu.
Chorus:
Naendelea mbele, naendelea mbele,
Sirudi nyuma tena, naenda na Yesu.[Repeat]
Verse 2:
Kama si wewe Yesu, ningekuwa wapi,
Ebeneza Mungu wangu, umenitoa mbali,
Nami nimeamua, takufuata milele,
Baba Yangu we, usiniache naenda.
Chorus:
Naendelea mbele, naendelea mbele,
Sirudi nyuma tena, naenda na Yesu.[Repeat]
Verse 3:
Umeniumba mimi, kwa umbo lako Yesu,
Menipa Ujasiri, wa Roho wako Mungu,
Ninaweza yote, wewe waniwezesha,
Sio kwa nguvu wala mamlaka, ni kwa Roho wako.
Chorus:
Naendelea mbele, naendelea mbele,
Sirudi nyuma tena, naenda na Yesu.[Repeat]
Verse 4:
Watoto vijana twende, wamama wazee twende,
Kenya yote twende, twende kwa Yesu,
Uropa Asia twende, Afrika yote twende,
Dunia nzima twende, twende kwa Yesu,
Kanisa lote twende, watoto wote twende.[repeat]
Chorus:
Naendelea mbele, naendelea mbele,
Sirudi nyuma tena, naenda na Yesu.[Repeat]