ads

Monday 9 January 2017

MATOKEO - GLORIA MULIRO











Sasa nangoja matokeo,
Kutoka kwako jalali.

Mimi nimefanya mitihani mingi sana,
Nimepitia madarasa mengi sana,
Kwa kila darasa Yahweh,
Umekuwa mwalimu wangu,
Umenifunza kuomba, umenifunza subira,
Umenifunza kungoja Baba,
Nimekuwa mwanafunzi mwema kwako Baba.

CHORUS:
Sasa nangoja matokeo,
Kutoka kwako jalali. [REPEAT]

Usiku mrefu sana, mbona hakupambazuki?
Nimejaribu sana kukupendeza maishani mwangu,
Nimefanya kazi, hiyo umeona Yesu,
Nimetoa fungu la kumi hiyo umeona Baba,
Nangojea, nangojea matokeo yangu,
Ulisema nikitoa, nitabarikiwa.

CHORUS:
Sasa nangoja matokeo,
Kutoka kwako jalali. [REPEAT].

Asubuhi ikifika, ije na kicheko,
Asubuhi ikifika, ije na amani,
Asubuhi ikifika, ije na furaha,
Asubuhi ikifika, ije na jibu langu.

CHORUS:
Sasa nangoja matokeo,
Kutoka kwako jalali. [REPEAT]





www.gospelyrix.com







No comments:

Post a Comment