ads

Monday 9 January 2017

NANI KAMA WEWE - GLORIA MULIRO











Ni nani kama wewe, x3
Mungu mkuu. [Repeat]

REFRAIN:
Kwa neno lako Bwana,
Uliumba dunia na vyote vilivyomo,
Jina lako Baba, limeinuliwa juu ya yote,
Hakuna, hakuna kama wewe.

(Refrain)

Uinuwae wanyonge,
Wawaketisha na wafalme,
Hakuna uwezaye tenda ila wewe,
Nikitazama maisha yangu,
Ulikonitoa Yesu wangu,
Nina sababu ya kusema, ni wewe pekee.

REFRAIN:
Kwa neno lako Bwana,
Uliumba dunia na vyote vilivyomo,
Jina lako Baba, limeinuliwa juu ya yote,
Hakuna, hakuna kama wewe.

Nani mwenye uwezo,
Nani mwenye rehema tele,
Nani mwenye enzi kama yako,
Ni wewe pekee,
Wastahili sifa zote,
Mbinguni na duniani Baba,
Twakusujudu, twakuabudu, twakuheshimu.

REFRAIN:
Kwa neno lako Bwana,
Uliumba dunia na vyote vilivyomo,
Jina lako Baba, limeinuliwa juu ya yote,
Hakuna, hakuna kama wewe.

Umetukuka adonai, el shadai,
Mungu mwenye nguvu,
Ni nani mwingine kama wewe,
Hakuna wa kulinganishwa na wewe Baba,
Nani kama wewe Baba/Yahweh.




www.gospelyrix.com







No comments:

Post a Comment