ads

Monday 9 January 2017

MTETEZI WANGU - CHRISTINA SHUSHO











Mtetezi wangu yesu anaishi leo,
[mtetezi wangu yu hai]
Ukienda kwa wanyama anaitwa simba wa yuda,
[mtetezi wangu yu hai]
Ukienda kwe miti anaitwa mti wa uzima,
[mtetezi wangu yu hai]
Ukienda kwenye maji anaitwa maji yalio hai,
[mtetezi wangu yu hai]
Wewe usiye na chakula yesu anaitwa mkate wa uzima,
[mtetezi wangu yu hai]
Ukifika kwenye miamba anaitwa mwamba imara,
[mtetezi wangu yu hai]
Hata kwa watawala yesu anaitwa mfalme wa wafalme
[mtetezi wangu yu hai]
Mtetezi x2 mtetezi wangu yu hai,
Mtetezi wamaisha,
Mtetezi wa kanisa,
Ukienda kwa wagonjwa anaitwa mponyaji,
[mtetezi wangu yu hai]
Hata wenye huzuni anaitwa mfariji,
[mtetezi wangu yu hai]
Uliye songwa na shida yeye anaitwa msaada,
[mtetezi wangu yu hai]
Mjane usifadhaike yesu anaitwa mume wa wajane,
[mtetezi wangu yu hai]
Yatima usilie yeye anaitwa baba wa yatima,
[mtetezi wangu yu hai]
Kwenye biashara yako muite mshauri wa ajabu,
[mtetezi wangu yu hai]
Ewe mama usilie na ndoa yako mama,
[mtetezi wako yu hai]
Ewe baba usilie umefukuzwa kazi,
[mtetezi wako yu hai]
Kijana usilie mchumba amekukataa,
[mtetezi wako yu hai]
Watumishi wa mungu msifadhaike,
[mtetezi wenu yu hai]
Fanye kazi ya mungu huyo aliye waiita,
[mtetezi wenu yu hai]
Hata kama mkisemwa na kutukanwa
[mtetezi wenu yu hai]





www.gospelyrix.com







No comments:

Post a Comment