ads

Monday 9 January 2017

MUNGU WA HURUMA - CHRISTINA SHUSHO











[Mungu wa huruma, utuhurumie,
ungehesabu maovu yetu, nani angesimama?] x2

toka mbinguni, Bwana alipochungulia mwanadamu,
aone kama ni mtu mwenye akili, amtafutaye Mungu
wote wamepotoka, wote wameoza,
hakuna atendaye mema ata mmoja, Mungu,
wapendwa tukikosana, tuonane kwa upendo,
wakubwa kwa wadogo, viongozi kwa viongozi,
watumishii.

CHORUS:
[Mungu wa huruma, utuhurumie,
ungehesabu maovu yetu, nani angesimama?] x2

dunia imeharibika sana,
uhovu mwingi kila mahali,
kama si neema yako, nani angesimama?

CHORUS:
[Mungu wa huruma, utuhurumie,
ungehesabu maovu yetu, nani angesimama?] x2

mwanadamu anaogopwa sana kuliko mnyama mkali,
kuaminiana hakupo tena, ndugu kusalitiana,
imani imetoweka, misingi imeharibika,
ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu,
watajinyenyekesha na kuomba,
na kutafuta uso, na kuliacha njia zao mbaya,
ntasikia toka mbinguni.

CHORUS:
[Mungu wa huruma, utuhurumie,
ungehesabu maovu yetu, nani angesimama?] x2





www.gospelyrix.com







No comments:

Post a Comment