ads

Monday 9 January 2017

MWEMA BY MERCY MASIKA











Wako mwana ukamtuma, duniani,
Kisa na maana nipate uzima jamani.

Ishara kwamba unanipenda zaidi,
Hivyo nishaelewa sifa nitakupa zaidi.

Refrain:
[Na siwezi jizuia, kusema wako wema,
Na sio kama najigamba, umenitenda mema.]X2
Umekuwa mwema kwangu.

Umenitoa gizani, nilipokuwa nimeshikwa mateka,
Ukanipa tumaini, kwako nikajificha,
Sasa nitakupa nini, iwe sawa na yale umenitenda?
Hakuna ila moyoni, sifa nitakuimbia.

Ilikugharimu, msalabani unifie,
Hivyo inanibidi, sifa nikuimbie,
Wema wako niseme, ili na wengine wakujue,
Wote waungane nami, na wazee ishirini na nne.

Refrain:
[Na siwezi jizuia, kusema wako wema,
Na sio kama najigamba, umenitenda mema.]X2
Umekuwa mwema kwangu.




www.gospelyrix.com







No comments:

Post a Comment