ads

Monday 9 January 2017

THAMANI YA WOKOVU WANGU - CHRISTINA SHUSHO

Ngoja nikusimulie, habari ya kijana mmoja,
Kijana mtanashati, mpole kipenzi cha wengi,
Anazo sifa nyingi lakini kuu kwake ni upendo,
Siku moja alikutana na mwanamke msamaria kisimani,
Kijana kamwomba maji, mwanamke naye kamuuliza,
Tangu lini wayahudi na wasamaria tukashikamana,
Kijana akamwambia ungejua mimi ni maji yaliyo hai,
Ungekuja kwangu unywe maji, ili usiwe na kiu tena.
Mimi aliniona nilikokuwa nimechoka, nimechakaa,
Kijana kanipenda, kanichukua kanitengenezaaa.

CHORUS:
Thamani ya Wokovu wangu
anayejua ni Mwokozi wangu,
Gharama ya maisha yangu
anayejua ni Muumba,
Nikisema nimeokokaa mbona
hamnielewiii,
Nikisema nimependwa mie, mbona
mwanishangaaa.

Maisha ni hazina, iliyo mikononi mwa Mungu,
Hakuna ajuaye, salio la siku zake,
Ukiona ni mzima leo, hujui kesho itakuwaje?
Ndiyo maana nimeona nikukumbushe habari za Yesu,
Yeye akikupenda, wala hatoitoi kasoro,
Ukimupokea leo anabadili historia yako,
Atakuchukua hivyo ulivyo akufanye kiumbe kipya,
Hata kama unalia leo jua kesho utacheka,
Huyu Mwanaume Yesu ni wa ajabu wala hana mfano wake,
Upendo wake ulivyo mkuu kwetu akajiona heri ajitoe,
Aliacha enzi na utukufu mbinguni,
Akakubali mateso hata kifo cha aibu,
Akavuliwa nguo, ili mimi nipone,
Akatemewa mate ili mimi niwe huru.

Chorus
Thamani ya Wokovu wangu
anayejua ni Mwokozi wangu,
Gharama ya maisha yangu
anayejua ni Muumba,
Nikisema nimeokokaa mbona
hamnielewiii,
Nikisema nimependwa mie,
mbona mwanishangaaa.

No comments:

Post a Comment