ads

Wednesday 14 March 2018

NALEGEA BY: ROSE MUHANDO







{Nalegea, wacha nichakae nje,
Lakini utu wangu wa ndani wa fanywa upya}x2
{Dhiki yangu ni nyepesi na ya muda,
Yaani fani wa utukufu wa milele} x2
{Nayahesabu mambo yote bure,
Kwa ajili ya jina la Yesu (Kristo)} x2

{Natazama, tena imeandikwa,
Ni mizuri kama nini – miguu yao} x2
{Wale wote wapelekeo habari njema,
Ya utukufu wa Yesu Kristo Bwana wangu} x2
{Nayahesabu mambo yote kama mavi/bure,
Kwa ajili ya uzuri wa Yesu (Kristo)} x2

Vipi mwenzangu, wanitazama?
Ninaposema habari zako,
Ninapotaja na mambo zako,
Wacha Makali, hasira nyingi,
{Wazielekeza juu yangu, bila sababu,
Na kumbe mimi ni mtumishi, niliyetumwa} x2

Nikikwambia uache dhambi,
Ushirikina, uchawi fitina,
Wanichukia, wanichukia,
{Lakini Bwana asema hivi, ni ole wenu,
Wanawake washonao hirizi viunoni mwao,
Wanaoroga kwa mafumbo, wasio na haya} x2

{Sikia, ewe mkaidi,
Ee mwenye shingo ya chuma,
Utavuna ulichopanda,
Mabaya yatakupata} x2

{Kumbuka ewe mshirikina:
Uzao wa mwanamke mchawi,
Mumeo atatwaliwa,
Wanao watabaki yatima,
Na uchawi, hautakusaidia} x2

{Ninawaangalia yatima,
Ninawafahamu wajane,
Nimesikia kilio chao,
Nimeyaona mateso yao} x2

{Lakini Yesu, amefukuka,
Dhambi, mauti hakuna tena,
Shetani kuzimu, anatetemeka} x2

{Eh Halleluya, sasa twashinda,
Mapendo yakimbia kwa jina lake} x2

Wewe, Yesu ni njia,
Wewe, Yesu ni uzima.




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







No comments:

Post a Comment