ads

Wednesday 14 March 2018

MUNGU WANGU BY: ROSE MUHANDO







E mungu wangu mimi ninatukushukuru,
Mbele ya mataifa mimi nitaimba,
Dunia nzima nayo itambue hilo,
Kwamba jina la yesu pekee ndilo,
Ulimwengu mzima uokolewe kwalo.

Asubuhi na mapema, mimi nitaimba,
Kabla ya kinywa kunena, kwako nitaimba,
Tufani ijapozidi wo, kwako nitaimba,
Nijapoteswa kabisa, kwako nitaimba,
Nijapodharauliwa, kwako nitaimba.

Chorus:
Swiyi… Sikia e kinanda,
Swiyi… Amka we kinubi,
Swiyi… Sikia e kinanda,
Inuka e zumari, inuka kwa sauti(x2)
Woo na utukuzwe Mungu, Woo na utukuzwe Mungu,
Yee Jehova adonai, Yee Jehova adonai,
El gibo shalom mungu unaitika
El gibo shalom mungu unaitika

Uniondolee majivuno, komesha kiburi,
Utawale akili zangu, Bwana niongoze,
Unifundishe roho yangu habari za mbingu,
Sikizeni eh kizazi changu, Mungu anaishi,
Uniondolee majivuno, komesha kiburi,
Utawale akili zangu, Bwana niongoze,
Unifundishe roho yangu habari za mbingu,
Sikizeni eh kizazi changu, Mungu anaishi.

Chorus:
Swiyi… Sikia e kinanda,
Swiyi… Amka we kinubi,
Swiyi… Sikia e kinanda,
Inuka e zumari, inuka kwa sauti(x2)
Woo na utukuzwe Mungu, Woo na utukuzwe Mungu,
Yee Jehova adonai, Yee Jehova adonai,
El gibo shalom mungu unaitika
El gibo shalom mungu unaitika.

NIpe moyo ya nyama, ulopondeka,
Moyo uliotulia, na unyeyekevu,
Mimi si kitu kwako, ni mdhuru? tu,
Mimi ni kama nani, uniinue,
Unifinyange bwana, kama upendavyo,
Unifundishe Bwana kama upendavyo.

Chorus:
Swiyi… Sikia e kinanda,
Swiyi… Amka we kinubi,
Swiyi… Sikia e kinanda,
Inuka e zumari, inuka kwa sauti(x2)
Woo na utukuzwe Mungu, Woo na utukuzwe Mungu,
Yee Jehova adonai, Yee Jehova adonai,
El gibo shalom mungu unaitika
El gibo shalom mungu unaitika

NIkikuita mungu, unaitika,
Rohi eloie heika (?), noishikimu (…Hebrew (?))
Jira el shadai, Jehova oseenu(…Hebrew (?))
El elyo shammah, Mungu unaitika,
Jehova shabbah, Mungu utanijibu,
El gibo shalom, Mungu unaitika,
El gibo shalom, Mungu unaitika,
El gibo shalom, Mungu unaitika.

Chorus:
Swiyi… Sikia e kinanda,
Swiyi… Amka we kinubi,
Swiyi… Sikia e kinanda,
Inuka e zumari, inuka kwa sauti(x2)
Woo na utukuzwe Mungu, Woo na utukuzwe Mungu,
Yee Jehova adonai, Yee Jehova adonai,
El gibo shalom mungu unaitika
El gibo shalom mungu unaitika






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







No comments:

Post a Comment