ads

Wednesday 14 March 2018

NIBEBE BY: ROSE MUHANDO







CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Verse 1:
E mungu angalia kunena kwangu,
Na usikie sauti ya kilio changu,
Moyo wangu umechoka sana baba,
Kwa ajili ya wingi wa mateso yangu,
Nafsi yangu imegandamana na mavumbi,
Niokoe mikononi mwa midomo ya mbwa,
Kwanini ninateswa sana kwa ajili yako babangu?
Niokoe mikononi mwa watu wabaya,
fanya hima unisaidie nibebe.

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Nimechoka peke yangu safari ngumu ni ndefu nibebe,

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Verse 2:
Macho yangu yamedhoofukwa machozi,
Kwani mateso yangu hayapimiki kwa mizani,
Kwa kuwa aliyenitukana siye adui yangu,
bali ni rafiki yangu tuliyejuana naye sana,
Tulikula pamoja, tulisali pamoja, kanisani pamoja,
Bwana asifiwe kwa sana,
Kumbe mwenzangu alikusudia kuniangamiza,

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Kweli nimeamini adui wa kwanza ni yule wa nyumbani mwako

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

verse 3:
Wengine wakinibeba nitaambulia matatizo, yesu nibebe,
Dunia ikinibeba itanipeleka jehanamu, yesu nibebe,
Marafiki wakinibeba watanipeleka pabaya, yesu nibebe,
Baba nibebe, yesu nibebe,
Nibembeleze nibebe, nichukue mbiguni salama.

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Nimechoka pekee yangu safari ngumu siwezi.

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

(verse 4)
Nifike mbinguni nimwone Eliya (Amen),
Nifike mbinguni nimwone Yakobo (Amen),
pamoja na kiti cha enzi mbinguni kwa baba,
Njia za dhahabu nami nakatembelee,
O baba nibebe, yesu nibebe,
Nibembeleze nibebe, nichukue mbiguni salama

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Nakwita Yesu unibebe mwokozi,

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Verse 5:
Nifike mbinguni nikamwone baba (Amen)
Nifike mbinguni nakapumzike (Amen),
Katika kiti cha enzi nami nikasujudie,
Niwaone wenzangu wale walionitangulia,
Nikale matunda ya mti wa uzima,
Yesu nibebe, baba nibebe,
Nibembeleze nibebe nichukue mbiguni salama.

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







No comments:

Post a Comment