ads

Wednesday 14 March 2018

MUNGU WA MAPENDO BY: ROSE MUHANDO







[Nini kitanitenganisha (na upendo wa Mungu Baba),
Ikiwa ni dhiki au njaa (Havitananitenga naye Baba),
Mauti, upanga, na dhihaka (Havitananitenga naye Baba)] X2

CHORUS:
[Sina hofu sibabaiki,
Kwake yeye nime/nitashinda,
Milele yote nime/nitashinda,
Tena zaidi ya kushinda,
Kwake yeye aliyenipenda.] X2

Kwenye zamu yangu nitasimama,
Kwa miguu yangu nitasimama,
Nione Bwana atakavyonijibu mimi,
Kwa habari ya kulalamika kwangu,
Bwana aliniambia neno hili,
“Usiogope maneno yao,
Usitetemeke mbele yao,
usifadhaike mbele yao,
Maana imeandikwa, kwa ajili yako ninauawa,
kama kondoo wa kuchinjwa, kifo nimehesabiwa,
Kifo nimehesabiwa, mimi sibabaiki

Bridge:
Shetani usinisumbue (Shetani usinisumbue)
Wala usinibababishe (Wala usinibababishe)
Funga kinywa ukatoweke (Funga kinywa ukatoweke)
Nyamaza kimya ukapotee (Kwa jina la Yesu ukatoweke)
Nyamaza kimya ukapotee (Nyamaza kimya ukapotee)

CHORUS:
[Sina hofu sibabaiki,
Kwake yeye nime/nitashinda,
Milele yote nime/nitashinda,
Tena zaidi ya kushinda,
Kwake yeye aliyenipenda.] X2

Milele neno la Mungu limehakikishwa,
Tena ni ngome kwa wamwaminio,
Tena ni ngao kwa wamwitao Baba,
Kabla ijawa misingi ya dunia,
Yeye huyu alikuweko,
muumba wa utukufu,
Na utakaso wa dhambi,
Nami kwake ni wa mwana x2, ni wa mwana,

Bridge:
Shetani usinisumbue (Shetani usinisumbue)
Wala usinibababishe (Wala usinibababishe)
Funga kinywa ukatoweke (Funga kinywa ukatoweke)
Nyamaza kimya ukapotee (Kwa jina la Yesu ukatoweke)
Nyamaza kimya ukapotee (Nyamaza kimya ukapotee)


CHORUS:
[Sina hofu sibabaiki,
Kwake yeye nime/nitashinda,
Milele yote nime/nitashinda,
Tena zaidi ya kushinda,
Kwake yeye aliyenipenda.] X2

Asifiwe Mungu wa mapendo
Asifiwe Mungu wa huruma
Asifiwe Mungu wa amani
Asifiwe Mungu wa mapendo
Asifiwe Mungu wa mapendo
Ametenda maajabu,
dunia ishangilie
Visiwa vitoe nyimbo,
Asifiwe Mungu wa mapendo
Mungua chukua heshima yako
Mungu chukua utukufu wako
Asifiwe Mungu wa mapendo
Ametenda maajabu,
dunia ishangilie
Visiwa vitoe nyimbo,
Asifiwe Mungu wa mapendo. X2




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







No comments:

Post a Comment