ads

Monday 9 January 2017

BADO NAKUNGOJA - CHRISTINA SHUSHO











Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi,
nayo inchi ilikua tupu,
gizi lilikua juu ya vilindi vya maji
roho ya Bwana ikatulia juu ya uso wa maji,
Mungu akasema iwe nuru ikawa nuru,
Mungu akaona nuru ya kuwa ni njema,
Mungu akaitenga nuru na giza,
Mungu akaita nuru mchana, giza usiku,
Mungu akasema na iwe na anga kati ya maji,
akayatenga maji na maji,
Mungu akaliita lile anga mbinguni
Mungu akapaita pale pakavu nchi
makusanyiko ya maji akayaita bahari,
mche utoa mbegu kwa jinsi yake,
mti uzao matunda na mbegu zimo ndani yake,
Mungu akayaona yote kuwa ni mema,
Mungu akasema na iwe na mianga,
itenge kati ya mchana na usiku,
iwe dalili ya siku na miaka,
Mungu akasema maji yajawe kwa wingi,
ndege waruke juu ya nchi,
Mungu akaumba nyangumi wakubwa,
akisema zaeni mkaongezeke,
ndege wazidi katika nchi,
Mungu akasema nchi izae kiumbe kwa jinsi yake,
Mungu akafanya mnyama wa mwitu na wa kufugwa
Mungu akasema wamfanye mtu,
kwa mfano wake na sura zetu,
wakawatawale samaki wa baharini na ndege wa angani,
wanyama wa nchi yote na pia kitaambacho,
kwa mfano Mungu aliumba mwanamume na mwanamke,
zamu yangu ya kungoja useme


Mungu akaona, kile alichofanya na tazamo, ni njema,
bado nakungoja,
kile alichosema kikatokea akaona ni njema,
bado nakungojaa,
nami nakungoja,
baba nakungoja useme na moyo,
bado nakungoja,
ukisema na moyo,
natiwa nguvu nasonga mbele kwakazi yako,
bado nakungoja,
sema na kanisa, sema na watu wako,
bado nakungoja,
ukisema leo wagonjwa watapona,
ukisema leo watasa watazaa,
bado nakungoja,
ukisema leo viziwi wasikie,
ukisema leo vipofu wataona,
bado nakungoja,
ukisema leo viwete watatembea,
ukisema leo mabubu watasema,
bado nakungoja,
sema na nchi,
sema na viongozi,
sema na taifa,
bado nakungoja,
ukisema leo hakuna vikao,
ukisema leo hakuna magomvi,
we Bwana kwako wanakuja wote,
kila mmoja na shida zake,
wamama na maskini wawe navyo nao wajitegemee,
bado nakungoja,
nimetambua kwamba una mengi niombayo kwako ni machache,
bado nakungoja,
bado nakungoja unifute machozi,
bado nakungoja unipe mwendo mpya,
bado nakungojaa,
mimi nakungoja utimize ahadi na kungoja,
bado nakungoja
Baba nangoja unijibu maombi,
bado nakungoja,
Baba nakungoja upoze wagonjwa wetu,
nakungoja Baba, nakungoja Baba,
bado nakungoja,
Baba nakungoja uwape matasa watoto,
nakungoja,
bado nakungoja,
Mungu useme neno kwa kuwa lina ukweli,
Bali neno lako ni kweli.





www.gospelyrix.com







No comments:

Post a Comment