ads

Monday 9 January 2017

LAZIMA USAMEHE - BAHATI BUKUKU











Unasema huwezi, huwezi, huwezi,
huwezi, x2
[naomba niseme yaliyonikuta,
naomba niseme niliyoyaona] x2

nilikua na rafiki yangu mzuri,
aliyeugua ugonjwa wa ajabu,
kwa huruma zangu nikamhurumia,
nikatumia muda wangu mwingi,
nkazunguka huku na kule kutafuta madaktari,
nikatembea huku na huko kutafuta uzima wake,
lakini Mungu sio mwanadamu alinihurumia,
akaachilia uzima moyoni mwake akawa mzima,
nikatafuta ata wachungaji nao wakamuombea,
nikatafuta wana maombi wakamuombea,
lakini Mungusi mwanadamu alinisikia,
niliposema Mungu mponye, alisikia,
kwa kuwa Mungu sio mwanadamu alimponya,
cha kushangaza alipopona, malipo yangu, x2
aligeuka adui yangu,
amekuwa msiba kwangu,
nasema siwezi, siwezi
siwezi, siwezi,
siwezi kumsamehe huyu, x2

[lazima usamehe ili Mungu akuinue,
lazima usamehe ili Mungu aseme nawe,] x4

naomba niseme yaliyonikuta,
naomba niseme yaliyonifika,
mimi mwenzenu,
kama wema ni uadui, basi umenifika,
kama wema ni uadui, basi ni zamu,
ameleta msiba, huyo,
ameuwa watoto wangu wangu, mimi mwenzenu,
ameleta kilio, huyo,
amevunja na ndoa yangu, mimi mwenzenu,
nasema siwezi, siwezi,
siwezi, siwezi,
siwezi kumsamehe huyu, x2
ni kweli umeumizwa wewe,
ni kweli umedharauliwa wewe,
ni kweli umekata tamaa wewe,
unasema huwezi, huwezi,
huwezi, huwezi,
lakini huo ndio ushindi wako,
anayeleta heshima ya jina lako,
huyo ndiye kazi ya kupandia wewe,
ili Mungu akuinue lazima ukutane naye,
unayo yapitia ili Mungu aseme nawe,
lazima adui wako wainuke, ili akuinue,
lazima ukutane naye unayepitia, ili Mungu aseme nawe,
ni lazima adui zako wainuke akuinue, mbele ya macho yako,
mbele ya macho yako,
ili Mungu akuinue ni lazima adui zako wainuke,
ni lazima ili Mungu akuinue,
ni lazima watu wapigane nawe,
ili Mungu akuinue, ni lazima ushuhuda wako utimie,
ili Mungu akuinue, ni lazima awatenge mbali wale adui zako,
ili Mungu akuinue, ni lazima apepete makapi kwanza,
ili wale wasio faa, lazima watajitenga na wewe,
wale ambao ni kusudi lake, watalia pamoja nawe,
ili Mungu ajitukuze ni lazima upitie majaribu,
ili Mungu akuinue, lazima ndugu wajitenge nawe.

CHORUS:
[lazima usamehe ili Mungu akuinue,
lazima usamehe ili Mungu aseme nawe,] x4




www.gospelyrix.com







No comments:

Post a Comment