ads

Monday 9 January 2017

NIPE MACHO - CHRISTINA SHUSHO











(Nipe macho nione,
macho eh eh
nipe macho nione sawasawa.)x4

nisaidie macho ya ndani,
nione jinsi uonavyo wewe,
nisaidie macho ya ndani,
nione mitego ya mwovu,
nimekukimbilia wewe Bwana,
ili nikae salama,
nipe macho nione, sawasawa,
mara nyingi watu watazama nje,
lakini wewe waona ndani,
kwa nje mtu huonekana mwema,
kumbe ndani ni hatari,
mwaka huu Bwana nataka nione
ili nikae salama,
nipe macho nione, sawasawa.

(Nipe macho nione,
macho eh eh,
nipe macho nione sawasawa.)x4

nipe macho nione,
kama alivyoona Stephano,
katika mazingira magumu,
akamwona Yesu amesimama mkono wa kiume wa Bwana,

macho yangu yanaona nimevaa,
kumbe waniona mtupu,
mara najiona ni tajiri,
kumbe waniona ni masikini,
mara nyingine macho yanipa haki,
kumbe waniona mkosaji,
nipe macho nione, sawasawa,
macho yangu yanaonaa nina nguvu,
kumbe waniona mnyonge,
tena najina na busara,
kumbe waniona mjinga,
macho yangu yaona ya usoni,
wewe waona mwisho kabla ya mwanzo.

(Nipe macho nione,
macho eh eh,
nipe macho nione sawasawa.)x4

[nipe macho ,
oh oh oh ohhhhh]x2

(Nipe macho nione,
macho eh eh,
nipe macho nione sawasawa.)x4




www.gospelyrix.com







No comments:

Post a Comment