ads

Monday 9 January 2017

TAABU ZANGU - CHRISTINA SHUSHO











Haleluya naitazamia mbingu mpya na nchi mpya
Huko nitapumzika milele
Taabu zangu zikiisha, nitamwona Bwana wangu
Akinikaribisha kule, karibu upumzike
Hapa ndipo nyumbani kwako, hapa ndipo mahali pako
Hapa ndipo makao yako, karibu upumzike
Haleluya nitaketi kwa furaha, nitapumzika kwa Mungu,
nitapumzika
Nitavikwa mavazi meupe, nitavikwa taji ya ushindi
Taabu zote na mateso yote, hakika vitakoma
Nitaungana na malaika, maserafi na makerubi
Tukiimba nyimbo za ushindi, haleluya usifiwe
Naona mbingu zimefunguka, na Yesu yu mkono wa kuume
[Akinitazama kwa upole, kwa macho yenye huruma] x2
Tatazama vidonda vyangu, tatazama makovu yangu
[Niloumizwa duniani, na watu wa ulimwengu.] x2
Tachukua kitambaa, atanifuta machozi,
Akisema pole mwanangu, Yesu tanikumbatia,
Bado kitambo kidogo, nitapumzika,
Yesu atanipeleka, kwenye kijito cha uhai,
Huko taniosha mwili wangu, nitapewa mwili mpya,
Nami nitaimba hosana, hosana ndiye mbarikiwa,
Nitaruka kama ndama, milele hata milele, X2
Tavumilia, kwa ajili yako Baba
Yatosha walivyokuonea, Yatosha walivyokudhulumu,
Yatosha walivyokupiga, karibu upumzike, x2
Yatosha walivyokuudhi, Yatosha walivyokutukana,
Yatosha walivyokuzomea, karibu upumzike, x2
Haleluya, mateso yangu yakiisha nitauona uso wa Mungu,
Nitamwona Yesu niliyepigwa kwa ajili yake,
Yatosha walivyokuonea, Yatosha walivyokudhulumu,
Yatosha walivyokupiga, karibu upumzike, x2
Yatosha walivyokuudhi, Yatosha walivyokutukana,
Yatosha walivyokuzomea, karibu upumzike, x2
Yesu atanipeleka, kwenye kijito cha uhai
Huko taniosha mwili wangu, nitapewa mwili mpya
Baada ya taabu, ni furaha





www.gospelyrix.com







No comments:

Post a Comment