ads

Thursday, 15 March 2018

ASANTE YESU BY: ANGELA CHIBALONZA




umbali tumetoka
na mahali tumefika
ndio maana ninatambua

kwamba wewe ni Ebenezer
sio kwa uwezo wangu
ila ni kwa uwezo wako
mahali nimefika baba
acha nikushukuru
eh bwana umenisaidia
nifike mahali nimefika
bwana wewe ni ebenezer
maishani mwangu ooh
mi nataka ebenezer
nijengwe juu yako
mi nataka ebenezer
uwe msingi wangu
jiwe langu la pemebeni
nakutamani sana
jiwe langu la thamani
nakuhitaji sana
ooh ebenezer
jiwe langu
mi nataka maisha yangu
yajengwe juu yako
mi nataka ndoa yangu
ijengwe juu yako baba
ndoa zilizojengwa juu yako yahwe
hazivunjiki kamwe
nyumba zilizojengwa juu yako yahwe
mi nataka uimbaji yangu baba
ujengwe juu yako
maana wewe ni sauti yangu
wewe ni uzima wangu
mi nataka ebenezer nijenge juu yako
mi nataka ebenezer uwe msingi wangu
jiwe langu la pembeni
nakutamani sana
jiwe langu la thamani
nakuhitaji sana
ooh ebenezer
jiwe langu
ebenezer nang'aa
libanga nangai ya telo
olekitya mapewolo papaa eeh
kati na bomo inang'a
zambe, nakumisi oh
mukote akokani na yooh
bisika na komilelo yahwe
ezali sena makasi na yooh
mi nataka ebenezer
nijenege juu yako
mi nataka ebenezer
uwe msingi wangu
jiwe langu la pembeni nakutamani sana
jiwe langu la thamani nakuhitaji sana
mi nataka ebenezer nijenge juu yako
mi nataka ebenezer uwe msingi wangu
jiwe langu la pembeni nakutamani sana
jiwe langu la thamani nakuhitaji sana
Ebenezer ni jiwe langu
jiwe langu la msingi
mahali nimefika leo, ni kwa ajili yako ebenezer
mawe mengi yako hapa chini ya jua
kuna dhahabu, kuna almasi
kuna mawe hata sijui majina yake
lakini hakutawahi kuwa jiwe
kama Ebenezer




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







ANAWEZA BY: ANGELA CHIBALONZA







Uliniumba nikuabudu (You created me to worship you)
Kwa ajili yako mimi naishi (Because of you I'm alive)
Pasipo wewe singekuwepo (Without you I would not be here)

Mimi ni kazi ya mikono yako (I am the work of your hands)
Baba ninaona nikuabudu (Father I prefer to worship you)
Maana matendo yako ni mengi sana (Because your works are many)
Ishara zako Baba ni nyingi mno (Your signs are many)
Maana wewe ndiye Mungu wangu (Because you are my God)
Uliniumba niseme matendo yako (You created me to tell of your actions)
Wewe ndiwe Mungu wa miungu (You are the God of gods)
Wewe kimbilio letu na ngome yet (You are our fortress and help)
Hakuna aliye kama wewe (There is no one like you)
Maneno ya kusema yananikosa (I am lost for words)
Maana matendo yako ni ya ajabu (Because your works are wondergul)
Maana ishara zako ni nyingi (Because your signs are many)
Kwa macho nimeona makuu yako (With my eyes I have seen your greatbess)
Masikio nimesikia matendo yako (My ears have heard your works)
Ndio maana nimetambua (That is why I know)
Ya kwamba niliumbwa nikuabudu (That I was created to worship you)
Mungu wa milele (Everlasting God)







Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







TABIBU BY: ANGELA CHIBALONZA







Nitabibu wa karibu
tabibu wa ajabu
na nehema na daima

ni dawa yake njema
hatufai kuwa hai
wala hatatumai ila yeye kweli ndiye
atupumzishaye

Imbeni malaika sifa
za Yesu Bwana
Pweke limetukuka Jina lake Yesu

Dhambi pia na hatia ametuchukulia
twenendeni na amani
hata kwake mbinguni
uliona tamu jina la Yesu Kristo Bwana
Yuna sifa mwenye kufa hasishindwe na kufa

Imbeni malaika sifa
za Yesu Bwana
Pweke limetukuka (limetukuka) Jina lake Yesu

Kila mume asimame
sifa zake zivume
wanawake na washike
kusifu jina lake

Imbeni malaika (sifa) sifa
za Yesu Bwana (ooh pweke)
Pweke limetukuka (limetukuka) Jina lake Yesu






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







JUBILEE BY: ANGELA CHIBALONZA







Eh Jubilee
Bongo tango yango oyo
To lamuka eh

Congo mboka na biso
Nzambe alingi biso mingi
Ye wana aza na nzela
Aza ko ya ko bikisa biso eh
Hallelujah
Bo fungola miso botala na ngomba

Leve toi. Soit elaire
Comme ta lumiere arive
Et la gloire de l'eternelle se leve sur toi
Ezali mbula ya jubilee
Bakonzi ya mboka bo lamuka eh

Ba Congolais, bolamuka eh
Belei ekoti na mboka ah
Mbula ya Nzambe eko noka eh
Bikuke ya Nzambe efungwami oh
Ezali mbula ya restoration

Jubilee, Jubilee
Oh Jubilee
Jubilee na Congo
Nzambe asili ko sala eh
Oh Jubilee
Jubilee, Jubilee
Oh Jubilee

Ba Congolais to sepela
Oh Jubilee
Nzambe ayoki mabondeli
Oh Jubilee

Oh Jubilee
Basali ya Nzambe telema
Bo kamba ba pate ya Nzambe eh
Bisika bilei bizali
Bato ya masumu tubela
bobanga Nzambe na Israel

Azali na makoki ya ko pambola
Soki afungoli nani ako kanga yango oh
Nzambe asili ko sala eh
Tika biso pe to lingana ah
To longola kanda na mitema
Jubilee, Jubilee
Oh Jubilee

Jubilee na Congo
Oh Jubilee
Mabala ekufa lamuka eh
Bolingo ekufa lamuka
Oh Jubilee
Economie ekufa lamuka ah
Oh Jubilee

Oh Jubilee, Jubilee
Oh Jubilee

Instrumental

Oh Jubilee
Soki Nzambe adimi nani ako boya eh
Soki Nzambe afungoli nani ako kanga ah
Oko tiya tembe
Oko mona kasi oko liya te

Nzambe asili ko sala ah
To longola elikya na Poto
To tiya elikia na Nzambe
To tonga mboka ya Congo
Kati na bomoko pe bolingo

Ba Congolais boyoka nga
Nzambe asili ko sala eh eh eh

Oh Jubilee
Jubilee, Jubilee
Oh Jubilee
Bato ya Goma bo sepela eh eh
Oh Jubilee

Volcan eyaki eko zonga pe
Oh Jubilee
Marchandise ekufaki eko telema eh
Commerce ekufaki lamuka
Oh Jubilee
Bolingo ekufaki lamuka
Oh Jubilee

Toyoka mongongo ya Nzambe eh
Hallelujah
Jubilee, Jubilee
Jubilee na Congo
Hallelujah

Nzambe atonda bolingo
Oh Jubilee
Nzambe atonda mawa, bandeko
Oh Jubilee
Alingi biso ba Congolais
Oh Jubilee

To sangana to tonga mboka na biso
Oh Jubilee
Ba president to lamuka eh
Oh Jubilee
Gouvernement to lamuka eh
Oh Jubilee

Hallelujah
Mwinda ya Nzambe epeli na Congo
Oh Jubilee




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







NINATAMANI BY: ANGELA CHIBALONZA







ninatamana nifanye mapenzi yake ili nifiki mbinguni kwa baba yangu
ninatamani niishi karibu naye ili ninywe maji ya uzima wa milele
yesu akasema mimi nimi njia ya uzima akuna awezae kufika kwa baba yangu bila kwangu mimi miminimi njia ya uzima

yesu akasema mimi nimi njia ya uzima akuna awezae kufika kwa baba yangu bila kwangu mimi miminimi njia ya uzima
baba natamani nikuone2
yesu natamani nikuone
masia natamani nikuone
maishani mwangu natamani nikuone
baba natamani nikuone

ninatamani niombe bila kukoma ili nifike mbinguni kwa baba yangu
ninatamani niyashinde majaribu
nivikwe taji, taji ya uzima wa milele

yesu akasema miminimkate wa uzima atakaye nila ataona kamwe njaa bali atakaa karibu nami milele2
baba natamani nikuone2
masia natamani nikuone
maishani mwangu natamani nikuone
kazini mwangu natamani nikuone
yesu natamani nikuone
baba natamani nikuone.




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







INUA MOYO WANGU BY: ANGELA CHIBALONZA







Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

Inua.

Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

Baba Inua.
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

(Instrumental)

Mara nyingi shida yasumbua moyoni, Mwanadamu huogopa na kunung'unika,
juu ya nini Mungu ameniacha lakini Bwana Yesu ni mwaminifu sana, lakini Bwana Yesu ni mwaminifu sana.

Inua
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

Bwana Yesu Inua.
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

Baba Inua
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

Instrumental

Jipe moyo Mwanadamu Bwana Yesu anakuona, anajua unapolala na unapoamkaaaa

Akiwa upande wako nani atakuwa juu yako... usiwe na wasiwasi linda imani yako, usiwe na wasiwasi linda imani yako.

Inua.
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

Bwana Yesu Inua.
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

Yesu Inua.
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

(Instrumental)

Kwa mganga wa kienyeji hakuna jibu lolote,
katika shida zangu na matatizo yangu,

Neno la Mungu lasema barikiwa mtu yule
anayemtumaini Mungu Baba Mwenyezi,
anayemtumaini Mungu Baba Mwenyezi...

Inua.
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

Bwana Yesu Inua.
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

Bwana Yesu Inua.
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

(Instrumental)

Baba Inua
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

Baba Inua.
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

Natamani kuzungumza na wewe.
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe,

Mimi nakuhitaji...
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe

Bwana Inua.
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe

Bwana Yesu inua.
Inua moyo wangu, ili mimi nizungumze nawe




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







KAA NAMI BY: ANGELA CHIBALONZA







Kaa nami ni usiku sana
Usiniache gizani bwana
Msaada wako haukomi
Nili pekee yangu, kaa nami

Siku zetu hazikawii kwisha
Sioni la kunifurahisha
Hakuna ambacho hakikomi
Usiye na mwisho, kaa nami

(Prayer)

Nina haja nawe kila saa
Sina mwingine wa kunifaa
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe bwana, kaa nami

Sichi neno uwapo karibu
Nipatalo lote si taabu?
Kifo na kaburi haviumi
nitashinda kwako, kaa nami

(Prayer)

Nilalapo nikuone wewe
Gizani mwote nimulikie
NUru za mbinguni hazikomi
Siku zangu zote kaa nami

(Prayer)






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







EBENEZAR BY: ANGELA CHIBALONZA







Umbali tumetoka, na mahali tumefika
Ndio maana ninatambua, kwamba wewe ni ebeneza
Sio kwa uwezo wangu,ila ni kwa uwezo wako
Mahali nimefika, acha nikushukuru
EE Bwana umenisaidia, nifike mahali nimefika
Bwana wewe ni ebeneza, maishani mwangu oo
Ninataka Ebeneza, nijenge juu yako
Ninataka Ebeneza, uwe msingi yangu
Jiwe langu la pembeni, nakutamani sana
Jiwe langu la thamani, nakuhitaji sana
Oo Ebeneza, jiwe langu

Ninataka maisha yangu, yajengwe juu yako
NInataka ndoa yangu, ijengwe juu yako baba
Ndoa zilizojengwa juu yako yahwe, hazivunjiki kamwe
Nyumba zilizojengwa juu yako yahweh hazivunjiki kamwe
Ninataka uimbaji wangu baba, ujengwe juu yako
Maana wewe ni sauti yangu, wewe ni uzima wangu

Ninataka Ebeneza, nijenge juu yako
Ninataka Ebeneza, uwe msingi yangu
Jiwe langu la pembeni, nakutamani sana
Jiwe langu la thamani, nakuhitaji sana
Oo Ebeneza, jiwe langu

Ebeneza na nga
libanga na ngai ya talo
oleki diamant mpe wolo papa eh kati na bomoyi na ngai
Nzambe nakumisi yo
moko te akokani na yo oh oh
Bisika nakomi lelo Yawe ezali nse na makasi na yo
Aleluya Nzambe na ngai

Ninataka Ebeneza, nijenge juu yako
Ninataka Ebeneza, uwe msingi yangu
Jiwe langu la pembeni, nakutamani sana
Jiwe langu la thamani, nakuhitaji sana
Oo Ebeneza, jiwe langu
Ebenezer ni jiwe langu, jiwe langu la msingi
Mahali nimefika leo, Ni kwa ajili yako ebeneza
Mawe mengi yako hapa chini ya jua
kuna dhahabu, kuna almasi Kuna mawe hata sijui majina yake
Lakini hakutawahi kuwa jiwe kama ebeneza






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







YAWEH UHIMIDIWE BY: ANGELA CHIBALONZA







Chorus:
Yahwe Uhimidiwe, (Yahweh be praised)
uaminifu wako umejulikana (Your faithfulness is known)
Kwa mataifa yote ya ulimwengu, Yahweh (By all the nations, Yahweh)
Yahwe Uhimidiwe, (Yahweh be praised)
uaminifu wako umejulikana (Your faithfulness is known)
Kwa mataifa yote ya ulimwengu, Yahweh (By all the nations, Yahweh)

Verse 1:
Uliumba lakini haukumbwa, (You created, but you were not created)
Jina lako jemedari, ninakuinua(You are the General, I lift you up)
Jina lako mkombozi, ninakupenda(You are the savior, I love you)
Umefuta jina langu kwenye hukumu(You have erased my name from the judgement)
Umefuta jina langu kwenye laana (You have erased my name from the curse)
Ndio maana ninakuina Mungu wangu ee(That is why I raise you up my God)
Kwa sababu siko tena chini ya dhambi ee(Because I am no longer under sin)

(Chorus)

Verse 2:
Kama si wewe Yesu ningeitwa nani?(If not for you Jesus, what would my name be?)
Kama si wewe Yesu Ningekuwa wapi?(If not for you Jesus, where would I be?)
Kama si wewe Yesu ningeenda wapi?(If not for you Jesus, where would I go?)
Kama si wewe Baba ningesema nini?(If not for you father, what would I say?)
Asante Bwana Yesu kwa ukombozi(Thank you Lord Jesus for the redemption)
Asante Bwana Yesu Kwa wokovu(Thank you Lord Jesus for the salvation)
Ndio maana nakuinua Mungu wangu(That is why I lift you up my God)
Umeniokoa mimi kwa damu ya bei(You have saved me from the price of blood)
Umenitendea mambo ya ajabu(You have done great things for me)
Ninakuinua Baba yahweh(I lift you up my father Yahweh)

(chorus)

Verse 3:
Majina yote mazuri ni yako baba(All the good names are yours father)
Unaitwa Jehova shammah, ninakupenda(You are Jehovah Shammah, I love you)
Unaitwa Jehova Jehova Jireh, ninakupenda(You are Jehovah Jireh, I love you)
Unaitwa Jehova Nissi bendera ya ushindi wangu(You are Jehova Nissi, my glorious banner)
Asante Baba yangu kwa upendo wako(Thank you my father for your love)
Hakuna Mwingine kama wewe(There is no one else like you)
Hakuna Mwingine kama wewe(There is no one else like you)
Ninakupenda Baba yangu(I love you my father)

(Chorus)




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







ULINIUMBA NIKUABUDU BY: ANGELA CHIBALONZA







Refrain:
Uliniumba nikuabudu (You created me to worship you)

Kwa ajili yako mimi naishi (Because of you I’m alive)
Pasipo wewe singekuwepo (Without you I would not be here)
Mimi ni kazi ya mikono yako (I am the work of your hands)

Baba ninaona nikuabudu (Father I prefer to worship you)
Maana matendo yako ni mengi sana (Because your works are many)
Ishara zako Baba ni nyingi mno (Your signs are many)
Maana wewe ndiye Mungu wangu (Because you are my God)
Uliniumba niseme matendo yako (You created me to tell of your actions)
Wewe ndiwe Mungu wa miungu (You are the God of gods)
Wewe kimbilio letu na ngome yet (You are our fortress and help)
Hakuna aliye kama wewe (There is no one like you)

Maneno ya kusema yananikosa ( I am lost for words)
Maana matendo yako ni ya ajabu (Because your works are wondergul)
Maana ishara zako ni nyingi (Because your signs are many)
Kwa macho nimeona makuu yako (With my eyes I have seen your greatbess)
Masikio nimesikia matendo yako (My ears have heard your works)
Ndio maana nimetambua (That is why I know)
Ya kwamba niliumbwa nikuabudu (That I was created to worship you)
Mungu wa milele (Everlasting God)

(Chorus)






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







Wednesday, 14 March 2018

YESU NAKUPENDA BY: ROSE MUHANDO







Chorus:
Yesu wee nakupenda, bwana yesu wee nakupenda,x2
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda,
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda,
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda,
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda,
Yesuuuu, yesu.

Msalabani dhambi zangu ulichukua,
Kufika kalivari Bwana ulizitua
Nami niwekwa huru ninakwimbia, (Repeat)

Nikufananishe na nani mwokozi wangu?
Naona fahari mimi ninakuimbia,
Nani asimame badala yako?
Hakuna mwingine ni wewe pekee yako.(Repeat)

Nafahamu Yesu anipenda mimi.

Chorus:
Yesu wee nakupenda, bwana yesu wee nakupenda,x2
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda,
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda,
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda,
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda,
Yesuuuu, yesu.

Nilipokuwa kwa shetani niliugua,
Ndugu na jamaa zangu walinikimbia,
Lakini yesu wa huruma ukanihurumia,
Nikufananishe na nani mwokozi wangu?
Naona fahari mimi ninakuimbia,
Nani asimame badala yako?
Hakuna mwingine ni wewe pekee yako.

Nafahamu Yesu anipenda mimi.

Chorus:
Yesu wee nakupenda, bwana yesu wee nakupenda,x2
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda,
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda,
Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda,
Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda,
Yesuuuu, yesu.


Kwimake eeh, kwimake weh,Kwimake weeh, kwimake eh
Kwimake mundewa Yesu,oh kwimake eh
kunilapa kwe ruhoma baba, oh kwimake weh
kunilapa kwe ruhoma baba, oh kwimake weh
Kwimake baba, kwimake baba, Kwimake baba, kwimake baba
Kwimake mundewa baba,oh kwimake eh
Jaga kyala, jaga kyala, jaga kyala baba, jaga kyala
Asante mwokozi wangu, uh asante eh,Asante mwokozi wangu, uh asante eh




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







UTAMU WA YESU BY: ROSE MUHANDO







Lile lile,

Acheni muone utamu wa Yesu we,
Mama we onjeni utamu wa Yesu we,
Mwenzenu nimeonja utamu wa Yesu we,
Usione nina raha nimeonja utamu wa Yesu we,
Si kama nimechanganyikiwa bali ni utamu wa Yesu we,
Jamani sijarukwa na akili bali utamu wa Yesu we,
Utamu we, nimeonja utamu we x2

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2
Utamu we, utamu x3
Utamu wa Yesu we, he
Mwemere, mwemere x4 (?)

Viko vingi vitamu lakini mwisho wake mauti,
Viko vingi vitamu lakini mwisho wake kilio,
Vingine ni vitamu lakini mwisho wake kilio,
Ni vitamu lakini mwisho vichungu kama shubiri,
Ni vitamu lakini mwisho vinawasha kama upupu,
Ni vitamu lakini mwisho vinapalia we,
Acheni niuseme utamu wa Yesu we,
Wacheni nisifu utamu wa Yesu we,
Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we,
Haufanani na utamu wa asali, utamu wa Yesu we,
Thamani yake imeshinda almasi, utamu wa Yesu we,
Ni mali ghafi isiopatika kwa mapesa jamani he,
Bali kwa njia ya msalaba tumepewa utamu wa Yesu we,
Mbinguni tunakwenda bure, uzima tunapata bure,
Wokovu tumepata bure, amani tunapata bure,
Utamu we, nimeonja utamu we x2

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2
Utamu we, utamu x3
Utamu wa Yesu we, he
Mwemere, mwemere x4 (?)

Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we,
Usione tuna raha, tumeonja utamu wa Yesu we,
Usione tunacheka, tumeonja utamu wa Yesu we,
Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we,
Umetusogeza karibu na Mungu, utamu wa Yesu we,
Dhambi zetu zimewekwa mbali na Mungu, utamu wa Yesu we,
Walio chini wameinuliwa, utamu wa Yesu we,
Badala ya kilio ni kicheko, utamu wa Yesu we,
Badala ya aibu utukufu, utamu wa Yesu we,
Mito ya baraka inatiririka, utamu wa Yesu we x2
Utamu we, nimeonja utamu we

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2
Utamu we, utamu x3
Utamu wa Yesu we, he
Mwemere, mwemere x4 (?)

Mkitaka magari mazuri, onjeni utamu wa Yesu we,
Mkitaka majumba mazuri, onjeni utamu wa Yesu we,
Mkitaka kubarikiwa, onjeni utamu wa Yesu we,
Mkitaka kuinuliwa, onjeni utamu wa Yesu we,
Utamu we, nimeonja utamu we.

Chorus:
Utamu we, nimeonja utamu we he x2
Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







UNASHANGAZA BY: ROSE MUHANDO







Tu-ru tururu tu-ru (?)

Matendo yako ya ajabu, yashangaza,
Fadhili zako za milele Baba, zashangaza,
Nikitazama ulivyoumba, ya shangaza,
Upendo wako kwangu mimi, yashangaza,
Miijuza na maajabu tele, washangaza,
Wanyama wa kondeni Baba, washangaza,
Milima na mabonde inaimba, washangaza,
Wanyama nao wanasema wewe washangaza,
Uumbaji wako Mungu, washangaza.

Matendo yako ya ajabu, washangaza,
Fadhili zako za milele Baba, zashangaza,
Uwezo wako kwa ulimwengu, washangaza,
Uumbaji wako wa pekee, washangaza,
Nikupe nini Mungu wangu? Washangaza,
Unavyonipigania Baba, washangaza,
Neema zako kwangu mimi, yashangaza.

Refrain: Ni wewe, ni wewe,
Mataifa waimba, niwewe,
Mbingu zaimba,
..?.. imba,
Jerusalemu waseme,
Mwenye nguvu ni wewe,
Mwenye uwezo ni wewe,
Wateule na waimbe,
..?.. imba,
..?.. imba,
Wateule imbeni,
Mwenye nguvu ni wewe,
Mwenye uwezo ni wewe,
Mwenye mamlaka,
Mungu nani kama wewe?






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







NIPISHE NIPITE BY: ROSE MUHANDO







Verse 1:
Nakuuliza shetani umepata wapi mamlaka,
Ya kukamata akili za watu,
Wewe umeleta balaa umeingia makanisani,
Umekamata wababa wanabaka watoto wao,
Umekamata vijana umewatwika ulevi,
Bila kusahau kina mama, vikao vya masengenyo,
Sasa nimechoka na mambo yako,
Ewe shetani, nipishe nipite.

Chorus:
Wewe ulimwasi mungu, nipishe nipite,
Uliwadanganya adamu na Eva, songea nipite,
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako,
WEwe ulimwasi mungu, nipishe nipite,
Uliwadanganya Adamu na Eva, songea nipite,
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako,
wewe shetani unaambiwa, mwenyeji wa kuzimu,
Sasa nipishe nipite.

Verse 2:
Hebu nipishe nipite, ninachelewa njiani,
Yesu yu karibu kurudi, kulichukua kanisa,
Kanda unayo nionyesha yote yamepitwa na wakati,
Huna ujanja,
Kumbuka miaka elfu mbili iliyopita zamani,
Yesu aliposhuka kuzimu, akakunyanganya funguo,
Funguo za mamlaka,
Nasema nimechoshwa na mambo yako,
Wewe shetani nipishe nipite.

Chorus:
Wewe ulimwasi mungu, nipishe nipite,
Uliwadanganya adamu na Eva, songea nipite,
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako,
WEwe ulimwasi mungu, nipishe nipite,
Uliwadanganya Adamu na Eva, songea nipite,
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako,
wewe shetani unaambiwa, mwenyeji wa kuzimu,
Sasa nipishe nipite.

Verse 3:
Nakuamuru shetani wewe, nipishe nipite,
Wewe umekuwa ni kikwazo kwangu, Kufika mbinguni,
Muda wako umeshakwisha, songea nipite,
Sasa haleluya naenda mbinguni, hakuna mashaka.
(Repeat)

Verse 4:
Wewe ulishaaniwa, laana milele,
Ulinyanganywa mamlaka na Yesu, Huna ujanja ee,
Simba wa yuda aliponguruma, mafuriko kuzimu,
Sasa haleluya twaenda mbinguni, hatuna mashaka.
(Repeat)

Chorus:
Wewe ulimwasi mungu, nipishe nipite,
Uliwadanganya adamu na Eva, songea nipite,
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako,
WEwe ulimwasi mungu, nipishe nipite,
Uliwadanganya Adamu na Eva, songea nipite,
Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako,
wewe shetani unaambiwa, mwenyeji wa kuzimu,
Sasa nipishe nipite.






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







NALEGEA BY: ROSE MUHANDO







{Nalegea, wacha nichakae nje,
Lakini utu wangu wa ndani wa fanywa upya}x2
{Dhiki yangu ni nyepesi na ya muda,
Yaani fani wa utukufu wa milele} x2
{Nayahesabu mambo yote bure,
Kwa ajili ya jina la Yesu (Kristo)} x2

{Natazama, tena imeandikwa,
Ni mizuri kama nini – miguu yao} x2
{Wale wote wapelekeo habari njema,
Ya utukufu wa Yesu Kristo Bwana wangu} x2
{Nayahesabu mambo yote kama mavi/bure,
Kwa ajili ya uzuri wa Yesu (Kristo)} x2

Vipi mwenzangu, wanitazama?
Ninaposema habari zako,
Ninapotaja na mambo zako,
Wacha Makali, hasira nyingi,
{Wazielekeza juu yangu, bila sababu,
Na kumbe mimi ni mtumishi, niliyetumwa} x2

Nikikwambia uache dhambi,
Ushirikina, uchawi fitina,
Wanichukia, wanichukia,
{Lakini Bwana asema hivi, ni ole wenu,
Wanawake washonao hirizi viunoni mwao,
Wanaoroga kwa mafumbo, wasio na haya} x2

{Sikia, ewe mkaidi,
Ee mwenye shingo ya chuma,
Utavuna ulichopanda,
Mabaya yatakupata} x2

{Kumbuka ewe mshirikina:
Uzao wa mwanamke mchawi,
Mumeo atatwaliwa,
Wanao watabaki yatima,
Na uchawi, hautakusaidia} x2

{Ninawaangalia yatima,
Ninawafahamu wajane,
Nimesikia kilio chao,
Nimeyaona mateso yao} x2

{Lakini Yesu, amefukuka,
Dhambi, mauti hakuna tena,
Shetani kuzimu, anatetemeka} x2

{Eh Halleluya, sasa twashinda,
Mapendo yakimbia kwa jina lake} x2

Wewe, Yesu ni njia,
Wewe, Yesu ni uzima.




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







MUNGU WANGU BY: ROSE MUHANDO







E mungu wangu mimi ninatukushukuru,
Mbele ya mataifa mimi nitaimba,
Dunia nzima nayo itambue hilo,
Kwamba jina la yesu pekee ndilo,
Ulimwengu mzima uokolewe kwalo.

Asubuhi na mapema, mimi nitaimba,
Kabla ya kinywa kunena, kwako nitaimba,
Tufani ijapozidi wo, kwako nitaimba,
Nijapoteswa kabisa, kwako nitaimba,
Nijapodharauliwa, kwako nitaimba.

Chorus:
Swiyi… Sikia e kinanda,
Swiyi… Amka we kinubi,
Swiyi… Sikia e kinanda,
Inuka e zumari, inuka kwa sauti(x2)
Woo na utukuzwe Mungu, Woo na utukuzwe Mungu,
Yee Jehova adonai, Yee Jehova adonai,
El gibo shalom mungu unaitika
El gibo shalom mungu unaitika

Uniondolee majivuno, komesha kiburi,
Utawale akili zangu, Bwana niongoze,
Unifundishe roho yangu habari za mbingu,
Sikizeni eh kizazi changu, Mungu anaishi,
Uniondolee majivuno, komesha kiburi,
Utawale akili zangu, Bwana niongoze,
Unifundishe roho yangu habari za mbingu,
Sikizeni eh kizazi changu, Mungu anaishi.

Chorus:
Swiyi… Sikia e kinanda,
Swiyi… Amka we kinubi,
Swiyi… Sikia e kinanda,
Inuka e zumari, inuka kwa sauti(x2)
Woo na utukuzwe Mungu, Woo na utukuzwe Mungu,
Yee Jehova adonai, Yee Jehova adonai,
El gibo shalom mungu unaitika
El gibo shalom mungu unaitika.

NIpe moyo ya nyama, ulopondeka,
Moyo uliotulia, na unyeyekevu,
Mimi si kitu kwako, ni mdhuru? tu,
Mimi ni kama nani, uniinue,
Unifinyange bwana, kama upendavyo,
Unifundishe Bwana kama upendavyo.

Chorus:
Swiyi… Sikia e kinanda,
Swiyi… Amka we kinubi,
Swiyi… Sikia e kinanda,
Inuka e zumari, inuka kwa sauti(x2)
Woo na utukuzwe Mungu, Woo na utukuzwe Mungu,
Yee Jehova adonai, Yee Jehova adonai,
El gibo shalom mungu unaitika
El gibo shalom mungu unaitika

NIkikuita mungu, unaitika,
Rohi eloie heika (?), noishikimu (…Hebrew (?))
Jira el shadai, Jehova oseenu(…Hebrew (?))
El elyo shammah, Mungu unaitika,
Jehova shabbah, Mungu utanijibu,
El gibo shalom, Mungu unaitika,
El gibo shalom, Mungu unaitika,
El gibo shalom, Mungu unaitika.

Chorus:
Swiyi… Sikia e kinanda,
Swiyi… Amka we kinubi,
Swiyi… Sikia e kinanda,
Inuka e zumari, inuka kwa sauti(x2)
Woo na utukuzwe Mungu, Woo na utukuzwe Mungu,
Yee Jehova adonai, Yee Jehova adonai,
El gibo shalom mungu unaitika
El gibo shalom mungu unaitika






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







NAKAZA MWENDO BY: ROSE MUHANDO







Nafurahia mateso yangu, nafurahia mateso yangu,
Ujapoharibika mwili huu, tapata mwingine kwa Baba,
Ujapoharibika mwili huu, tapata mwingine kwa Baba.

Chorus:
Nakaza mwendo, nifike Mbinguni,
Nayakabidhi, maisha kwa Bwana,
Nauone, uzuri wa bwana.x2

Taabu na matatizo, hakuna,
Kiu wala njaa, hakuna.x2

Verse 2:
Lakini mji ule taa yake, ni mwana kondoo,
Milele mji ule hauitaji, jua wala mwezi.

Najua kuishi kwangu ni pigo, kufa ni faida,

Chorus:
Nakaza mwendo, nifike Mbinguni,
Nayakabidhi, maisha kwa Bwana,
Nauone, uzuri wa bwana.x2

Verse 3:
Lakini waongo na wazinzi, hawataingia,
wala waabudu sanamu, hawataingia.x2

Najua kuishi kwangu ni pigo, kufa ni faida,

Chorus:
Nakaza mwendo, nifike Mbinguni,
Nayakabidhi, maisha kwa Bwana,
Nauone, uzuri wa bwana.x2






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







KIATU KIVUE BY: ROSE MUHANDO







Mungu alinena naye Musa hicho kiatu kivue,
Mungu alinena naye Musa hicho kiatu kivue,
Ulichotoka nacho kwa farao nakwambia,
Pahali hapa ni patakatifu hicho kiatu kivue. (x2)

Musa hicho kiatu, Musa hicho kiatu,
Nataka ninene nawe, nataka nikutumie,
Nataka nikuinue, nataka nikubariki,
Watu wangu waangamia,taifa langu la Israeli,
Watu wangu wanasononeka,watu wangu wanateseka,
Nataka nikutumie wewe, ukaokoe taifa langu we.

Hata leo mungu anena nasi hicho kiatu we,
Kiatu ni dhambi uzifanyazo ninakwambia,
Ukahaba unaoeneza kando kando ni kiatu,
Wivu na masengenyo vimekuja ni kiatu,
Kitakupeleka jehanamu hicho kiatu,
Kitakupeleka motoni wewe hicho kiatu,
Uzinzi unaoeneza wewe ni kiatu,
Uvalie wake wa wenzio magoti we nakwambia,
Utongoza waume wa wenzio ni kiatu we,
Kitakupekea jehanamu hicho kiatu,
Mama hicho kiatu, baba hicho kiatu,
Nataka ninene nawe, maana ninakupenda,
Nataka ninene nawe, ili nikuokoe,
Mimi sitaki uangamie, mimi sitaki upotee,
Mimi sitaki uangamie, maana mimi ninakujali,
Mimi Mungu ni wa neema, mimi mungu ni wa upendo.

Ukitaka Mungu akubariki lazima kiatu kivue,
Ukitaka kuinuliwa wewe ni lazima kivue,
Wivu ulio nao wewe ni lazima kivue,
Hutaki kuona mwenzako mama akiinuliwa wewe,
Hutaki kuona mwenzako akiwa amependeza,
Hutaki kuona mwenzako akiwa yuko smart,
Tabia ulio nayo mama ninakwambia wewe,
Hutaki kuona ndoa ya mwenzako jamani mke na mume wakicheka,
Tabia uliyo nayo baba, nakwambia badilika,
Hutaki kuona huduma ya mwenzako jamani likisonga mbele,
Hebu kivue, jamani hebu kivue,
Kiatu cha nyumba ndogo, kiatu cha ulevi,
Kiatu cha uzinzi, kiatu cha masengenyo,
Kivue, kivue, kivue, kivue.

Mungu ananena nawe hicho kiatu kivue,
Mungu anena nawe hicho kiatu kivue,
Valia mini waume wa wenzio iwe mwisho,
Kuvalia vitovu waume wa wenzio iwe mwisho,
Kupaka wanja kwa waume wa wenzio iwe mwisho,
Nataka nikupe mumueo, nataka nikupe nyumba yako,
Nataka nikuinue, nataka nikuinue,
Nataka nikuinue, niinue mume wako,
Niinue nyumba yako, nimwunue mke wako,
Nikupatia mchumba, kiatu cha nyumba ndogo,
Mungu anasema nawewe hicho kiatu kivue,
Kivue, kivue, kivue, kivue,
Ah, hicho kiatu kivue






Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







UTUKUZWE BY: ROSE MUHANDO







Ee Mungu utukuzwe, milele na milele,
Tena uinuliwe, katika mataifa yote,
Ee Mungu utukuzwe, milele na milele,
Ee Mungu uinuliwe, milele na milele,
Tena uhimidiwe katika mataifa yote,
Jina lako la ajabu, Wewe utishaye kuliko. x2

Wala haufanananishwi na chochote,
Jina lako Baba la ajabu.

Refrain:
Wewe uliupiga mwamba (maji yakabubujika),
Katikakati ya jangwa (wewe ulifanya njia),
Walipokumbana na adui (Wewe uliwapigania)
Wakafika (Kule Kanaani salama) X2
Usifiwe, utukuzwe, x2
Utukufu ni wako, milele na milele X2

Haya visiwa na viimbe,
Mito na ipige makofi,
Ndege na waseme amina kubwa,
Wanyama wa mwitu wasifu, X2
Bwana anatawala/Maana unatawala, wewe Bwana,
Heshima na enzi ni vya Bwana,
Utukufu na nguvu ni vya Bwana,
Umeketi mkono wenye nguvu, X2

Refrain:
Wewe uliupiga mwamba (maji yakabubujika),
Katikakati ya jangwa (wewe ulifanya njia),
Walipokumbana na adui (Wewe uliwapigania)
Wakafika (Kule Kanaani salama) X2
Usifiwe, utukuzwe, x2
Utukufu ni wako, milele na milele X2

Heshima ni yako (milele na milele),
Utukufu ni wako (milele na milele),
Heshima ni yako (milele na milele),
Mamlaka ina wewe (milele na milele),
Malaika waimbe (milele na milele),
Wazee ishirini na nne waseme (milele na milele),
Na wale wenye uhai waimbe (milele na milele),
Na watakatifu waseme (milele na milele).




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







SITANYAMAZA BY: ROSE MUHANDO







Eeeehhhh…. Mimi Mungu (Me, God)
Matendo nitalia, Kwa sinani nitaomboleza
Sodoma nitanung’unika, Mipakani nitashambulia
Mijini wameniacha,Kila mara nitashambulia
Maisha ya wanadamu, Yamenichosha….

Oh oh mimi
Sitanyamaza, wala sitanyamaza
Lakini nitalipa ujira wa vifuani mwao
Maovu yenu ninyi, pamoja na baba zenu
nasema nitalipa ndio mjue mimi ni Bwana
Mmefukiza uvumba, na kunitukana
Kwa ajili ya haya mtajutia vitani mwenu?(repeat)

mmefanya uzinzi katikati ya milima
Usiku wa manane mmefanya ukahaba
Kwenye njia kuu na vichochoro mmefanya mapatano
Kwenye mialoni na mipera mmefanya machukizo (repeat)

Ulitumaini uzuri wako ukafanya ukahaba
Kila kijana aliyepita ulimwona anafaa
Awe mzuri na sura mbaya ulifunua marinda

Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda
Wako wapi mapenzi zako mbona sasa unakonda
Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda
Wako wapi waelizamu (?) wako mbona sasa unakonda

Miji mizuri imekuwa ukiwa
Majumba mazuri yamefungwa kabisa
Wana wa wana wamebaki yatima
Kiburi chamuwamu(?) imekoma kabisa (repeat)

Hebu sasa piga kelele uliye kahaba,
Shika kinubi omboleza upate kukumbukwa (repeat)

Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye
Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye (repeat)

Lakini Bwana asema hivi, nitawaponya
Yeye mwenyewe aahidi, nitawabariki
Mimi ni alfa na omega, mwanzo na mwisho
Jamani mimi ni mungu, mwingine hapana

Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye (repeat)




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







NYOTA YA AJABU BY: ROSE MUHANDO







ILe nyota ya ajabu, yaonekana mashariki
Imejaa ishara zote, za kuzaliwa mfalme
Mamajuzi wako nyuma, kuifuata nyota ile
walifika Yerusalemu, nao wakauliza (repeat)
Yuko wapi yeye aliyezaliwa,
mtawala wa wayahaudi ili tumsujudie

Chorus:
Mjini mwa Daudi, amezaliwa mkombozi
Atakayewaokoa watu na dhambi zao
Dunia shangilieni, amezaliwa messiah
Haleluya haleluyah, sifa ni kwa Bwana

Verse 2:

Walikuwako na wachungaji, waliokaa makondeni
Wakilinda kundi lao kwa zamu usiku
Malaika kawatokea, kawambia msiogope
Maana leo katika Yuda, amezaliwa messiah

Chorus:
Mjini mwa Daudi, amezaliwa mkombozi
Atakayewaokoa watu na dhambi zao
Dunia shangilieni, amezaliwa messiah
Haleluya haleluyah, sifa ni kwa Bwana

Verse 3:
Walipokwisha kusema haya, Malaika wa bwana
Waliimba wimbo ule, wimbo usio na mwisho
Utukufu juu kwa Mungu mbinguni
Duniani we amani kwa aliowaridhia

Chorus:
Mjini mwa Daudi, amezaliwa mkombozi
Atakayewaokoa watu na dhambi zao
Dunia shangilieni, amezaliwa messiah
Haleluya haleluyah, sifa ni kwa Bwana

Verse 4:
Maongeo enzi yake, na tena begani mwake
Tazameni anakuja kwa jina lake Bwana
Maongeo enzi yake, na tena begani mwake
Tazameni anakuja kwa jina lake Bwana

Chorus:
Mjini mwa Daudi, amezaliwa mkombozi
Atakayewaokoa watu na dhambi zao
Dunia shangilieni, amezaliwa messiah
Haleluya haleluyah, sifa ni kwa Bwana




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







NIBEBE BY: ROSE MUHANDO







CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Verse 1:
E mungu angalia kunena kwangu,
Na usikie sauti ya kilio changu,
Moyo wangu umechoka sana baba,
Kwa ajili ya wingi wa mateso yangu,
Nafsi yangu imegandamana na mavumbi,
Niokoe mikononi mwa midomo ya mbwa,
Kwanini ninateswa sana kwa ajili yako babangu?
Niokoe mikononi mwa watu wabaya,
fanya hima unisaidie nibebe.

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Nimechoka peke yangu safari ngumu ni ndefu nibebe,

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Verse 2:
Macho yangu yamedhoofukwa machozi,
Kwani mateso yangu hayapimiki kwa mizani,
Kwa kuwa aliyenitukana siye adui yangu,
bali ni rafiki yangu tuliyejuana naye sana,
Tulikula pamoja, tulisali pamoja, kanisani pamoja,
Bwana asifiwe kwa sana,
Kumbe mwenzangu alikusudia kuniangamiza,

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Kweli nimeamini adui wa kwanza ni yule wa nyumbani mwako

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

verse 3:
Wengine wakinibeba nitaambulia matatizo, yesu nibebe,
Dunia ikinibeba itanipeleka jehanamu, yesu nibebe,
Marafiki wakinibeba watanipeleka pabaya, yesu nibebe,
Baba nibebe, yesu nibebe,
Nibembeleze nibebe, nichukue mbiguni salama.

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Nimechoka pekee yangu safari ngumu siwezi.

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

(verse 4)
Nifike mbinguni nimwone Eliya (Amen),
Nifike mbinguni nimwone Yakobo (Amen),
pamoja na kiti cha enzi mbinguni kwa baba,
Njia za dhahabu nami nakatembelee,
O baba nibebe, yesu nibebe,
Nibembeleze nibebe, nichukue mbiguni salama

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Nakwita Yesu unibebe mwokozi,

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.

Verse 5:
Nifike mbinguni nikamwone baba (Amen)
Nifike mbinguni nakapumzike (Amen),
Katika kiti cha enzi nami nikasujudie,
Niwaone wenzangu wale walionitangulia,
Nikale matunda ya mti wa uzima,
Yesu nibebe, baba nibebe,
Nibembeleze nibebe nichukue mbiguni salama.

CHORUS:
Nibebe nibebe nibebe nibebe,
Nibembeleze nibebe,
Nichukue unibebe,
Mikononi mwako niwe salama.




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







MUNGU WA MAPENDO BY: ROSE MUHANDO







[Nini kitanitenganisha (na upendo wa Mungu Baba),
Ikiwa ni dhiki au njaa (Havitananitenga naye Baba),
Mauti, upanga, na dhihaka (Havitananitenga naye Baba)] X2

CHORUS:
[Sina hofu sibabaiki,
Kwake yeye nime/nitashinda,
Milele yote nime/nitashinda,
Tena zaidi ya kushinda,
Kwake yeye aliyenipenda.] X2

Kwenye zamu yangu nitasimama,
Kwa miguu yangu nitasimama,
Nione Bwana atakavyonijibu mimi,
Kwa habari ya kulalamika kwangu,
Bwana aliniambia neno hili,
“Usiogope maneno yao,
Usitetemeke mbele yao,
usifadhaike mbele yao,
Maana imeandikwa, kwa ajili yako ninauawa,
kama kondoo wa kuchinjwa, kifo nimehesabiwa,
Kifo nimehesabiwa, mimi sibabaiki

Bridge:
Shetani usinisumbue (Shetani usinisumbue)
Wala usinibababishe (Wala usinibababishe)
Funga kinywa ukatoweke (Funga kinywa ukatoweke)
Nyamaza kimya ukapotee (Kwa jina la Yesu ukatoweke)
Nyamaza kimya ukapotee (Nyamaza kimya ukapotee)

CHORUS:
[Sina hofu sibabaiki,
Kwake yeye nime/nitashinda,
Milele yote nime/nitashinda,
Tena zaidi ya kushinda,
Kwake yeye aliyenipenda.] X2

Milele neno la Mungu limehakikishwa,
Tena ni ngome kwa wamwaminio,
Tena ni ngao kwa wamwitao Baba,
Kabla ijawa misingi ya dunia,
Yeye huyu alikuweko,
muumba wa utukufu,
Na utakaso wa dhambi,
Nami kwake ni wa mwana x2, ni wa mwana,

Bridge:
Shetani usinisumbue (Shetani usinisumbue)
Wala usinibababishe (Wala usinibababishe)
Funga kinywa ukatoweke (Funga kinywa ukatoweke)
Nyamaza kimya ukapotee (Kwa jina la Yesu ukatoweke)
Nyamaza kimya ukapotee (Nyamaza kimya ukapotee)


CHORUS:
[Sina hofu sibabaiki,
Kwake yeye nime/nitashinda,
Milele yote nime/nitashinda,
Tena zaidi ya kushinda,
Kwake yeye aliyenipenda.] X2

Asifiwe Mungu wa mapendo
Asifiwe Mungu wa huruma
Asifiwe Mungu wa amani
Asifiwe Mungu wa mapendo
Asifiwe Mungu wa mapendo
Ametenda maajabu,
dunia ishangilie
Visiwa vitoe nyimbo,
Asifiwe Mungu wa mapendo
Mungua chukua heshima yako
Mungu chukua utukufu wako
Asifiwe Mungu wa mapendo
Ametenda maajabu,
dunia ishangilie
Visiwa vitoe nyimbo,
Asifiwe Mungu wa mapendo. X2




Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site







Tuesday, 20 February 2018

HATUA ZA MWENYE HAKI BY: CHRISTINA SHUSHO






Hatua za mwenye haki, zaongozwa naye bwana,
na Bwana ufurahia, njia zake wakati wote X2

Nakukabidhi Bwana, njia zangu zote,
pia nakutumaini, najua Bwana utafanya,
Ata nijapojikwaa, sitaanguka chini,
Bwana
utanishika
mkono na kunitengenezaX 2

Bwana nimetambua
unafanya kazi kwa siri ndani yangu.

umwangazia mtumishi wako , uso wako,
maana ninayatamani maagizo yako.
Elekeza hatua zangu, kwa neno lako,
uovu usije ukanimiliki X2

[Refrain]
Ongoza hatua zangu, (ee bwana) X2
Ongoza mwendo wangu, (ee bwana) X2



Download our Gospel lyrics Android App Here

Download Christina shusho lyrics Android App Here


Visit Our Information Technology Site





>